Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 11/8 uku. 32
  • “Hayo Hunichangamsha Nyakati Zote”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Hayo Hunichangamsha Nyakati Zote”
  • Amkeni!—1993
Amkeni!—1993
g93 11/8 uku. 32

“Hayo Hunichangamsha Nyakati Zote”

“SIJAPATA kuwaandikia kamwe, lakini ni lazima niwashukuru kwa makala nyingi zenye kugusa moyo na zenye uzito ambazo mmechapisha katika Mnara wa Mlinzi na Amkeni!

“Nimekuwa nikisoma magazeti haya tangu 1974, na tangu wakati huo yamekuwa chanzo cha mafundisho, faida, na shangwe. Hayo hunichangamsha nyakati zote. Mimi hushuka moyo sana, na nikichukua tu na kusoma toleo mojayapo la magazeti hayo, hali ya moyo wangu huwa bora zaidi. Pindi kwa pindi makala moja imenisaidia nishughulike na watu wengine kwa njia ifaayo zaidi na kuwa mwenye kuelewa hali zaidi. Yamenisaidia nijielewe mwenyewe.

“Yaonekana kwamba katika mwaka uliopita, makala nyingi sana yalinihusu, hasa zile za ‘Wanawake—Wanastahili Staha’ [Amkeni! Desemba 8, 1992] na ‘Msaada kwa Wazoelevu wa Kileo na Familia Zao’ [Amkeni! Mei 22, 1992, Kiingereza]. Nilitoka tu kupoteza mama yangu katika kifo, na mfululizo wenye kichwa ‘Mpendwa Anapokufa’ [Amkeni! Julai 22, 1992, Kiingereza] ulinisaidia sana.

“J. A., North Carolina, U.S.A.”

Ikiwa ungependa kupata habari zaidi juu ya magazeti hayo yenye msingi wa Biblia, tafadhali ona Mashahidi wa Yehova kwenye Jumba la Ufalme la mahali penu, au andika kwa kutumia anwani iliyoko karibu zaidi nawe iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki