Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 12/8 uku. 31
  • Kutumia Upepo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutumia Upepo
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutumia Nguvu za Upepo
    Amkeni!—1995
  • Kucheza Dansi Pamoja na Korongo
    Amkeni!—2003
  • Jitihada za Mwanadamu za Kutumia Upepo
    Amkeni!—2004
  • Njia Mpya za Kutokeza Nishati
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 12/8 uku. 31

Kutumia Upepo

KUJENGWA kwa mashine ya kwanza ya Uingereza ya kuendeshwa kwa nguvu za upepo kwa ajili ya matumizi ya kibiashara kulipata pigo dogo wakati kreni zilizokuwa zikitumiwa kujenga mashine za tabini zilipopeperushwa katika dhoruba kali, kulingana na gazeti The Independent la London.[1] Hata hivyo, kutumia upepo kwasemwa kuwa moja ya njia za haraka zaidi na yenye gharama ndogo zaidi za kufanyiza nguvu za umeme. Jambo bora hata zaidi ni kwamba hakufanyizi uchafuzi wa kikemikali utokanao kwa kuchoma vitu kama makaa-mawe.[2]

Ingawa nchi kadhaa za Ulaya—kama vile Denmark, Uholanzi, Ujerumani—pamoja na Kalifornia, hupendelea kutumia upepo ukiwa chanzo cha nishati mpya, si wote wahusikao na mazingira wanapendezwa na jambo hilo.[3] Baadhi yao hawataki sauti za panga zenye kuzunguka za mashine za tabini; wengine hawapendi sura zazo mbaya, hasa kama mashine hizo ziko katika maeneo mazuri ya asili.[4]

Hata hivyo, katika Uingereza, mojayapo nchi zenye upepo mkali zaidi katika Ulaya,[5] washauri wa serikali hupendelea nishati itokanayo na upepo kuwa “chanzo chenye kutumainiwa zaidi cha kutokeza nishati karibuni,” laripoti gazeti New Scientist.[6] Kwa upande mwingine, zijapokuwa gharama za juu zihusikazo, wale wanaochambua kujengwa kwa mashine hizo za tabini barani wapendekeza zijengwe mbali baharini, kwa kutumia winchi za kipekee badala ya kutumia kreni kusogeza vifaa hivyo vizito—kwa kutumia pepo za bahari zenye nguvu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki