Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 uku. 32
  • Dhamiri, Mbona Wanitesa?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Dhamiri, Mbona Wanitesa?
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 1/8 uku. 32

Dhamiri, Mbona Wanitesa?

“OH DHAMIRI yenye woga, jinsi unavyonisumbua!” Maneno hayo maarufu, yaliyosemwa na Mfalme Richard 3 katika mchezo wa Shakespeare uitwao kwa jina hilohilo, yaeleza majuto ambayo dhamiri ya kibinadamu yaweza kutokeza. Katika maisha halisi dhamiri imetaharakisha na kubadili maisha ya wengi.

Uwezo wa dhamiri ulitolewa kielezi na kisa cha hivi karibuni cha kijana Mwitalia. Kazi yake akiwa mlinzi ilihusisha kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha. Mambo yote yaliendelea vizuri hadi siku moja aliposhindwa na kishawishi na kuiba gunia lenye lire 300,000,000 [dola 240,000 za U.S.]. Kwa kuwa alikuwa akifanya kazi na wenzake wawili na ilikuwa vigumu kuamua ni nani kati yao aliyekuwa ameichukua, wote watatu waliachishwa kazi.

Yeye alificha fedha alizoiba, akikusudia kuzitumia baada ya mambo kutulia. Badala ya hivyo, mateso yasiyotazamiwa yalianza: Alishindwa kuacha kufikiri juu ya kuachishwa kazi kwa wafanyakazi wenzake wasio na hatia. Dhamiri yake haingeweza kumtuliza. Alishindwa kulala. Alishindwa kula. Akawa mgumu kushughulika naye.

Hatimaye, kwa kushindwa na hatia na kuchoshwa na mng’ang’ano wake wa ndani, alienda kwa polisi na kuwakabidhi hizo fedha zilizoibwa. Yeye aliwaambia: “Majuto yalikuwa mengi mno. Siwezi kuyavumilia zaidi!” Yeye aliongeza: “Afadhali kuwa gerezani na kuwa mwenye haki kuliko kuwa huru huku ukiwa na dhamiri inayokushtaki kuwa mwivi.”

Dhamiri ni zawadi ya Mungu kwa watu wote. Huenda ikatushtaki au ikatutuliza. Tunapoisikiliza, huenda ikatuokoa tusifanye makosa, huku tukipuuza makosa mazito. Kwa hiyo badala ya kupuuza midukuo yayo au kuenda dhidi yayo kwa kuudhika kama vile Mfalme Richard 3 wa Shakespeare alivyofanya, twapaswa kuthamini na kulinda dhamiri yetu.—Warumi 2:14, 15.

Ikiwa ungependa habari zaidi juu ya Biblia na shauri layo lenye kutumika, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova kwenye Jumba la Ufalme la mahali penu, au uandike ukitumia anwani iliyo karibu zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki