Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/8 uku. 32
  • Kilipunguza Sana Ngono za Ovyo-Ovyo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kilipunguza Sana Ngono za Ovyo-Ovyo
  • Amkeni!—1994
Amkeni!—1994
g94 2/8 uku. 32

Kilipunguza Sana Ngono za Ovyo-Ovyo

Mshauri kwenye chuo kikuu katika Oklahoma, U.S.A., aliripoti kwamba kile kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi kimefanya yaliyo juu. Mshauri huyo kwenye Chuo Kikuu cha Langston aliandika:

“Ningemshauri mtu yeyote anayeshughulika na vijana wenye umri kati ya miaka 13-18 atumie kitabu hiki hususa. Hicho hueleza ngono katika njia ambayo wanafunzi wetu wapaswa kuijua ili kukabiliana na matatizo ya jamii ya leo iliyotatana. Kutokana na ono langu mwenyewe, nilipata kwamba hicho huwasaidia kujua juu ya yale yanayoweza kuwapata ikiwa wanafanya ngono za ovyo-ovyo. Kinawafahamisha juu ya maradhi mbalimbali yanayopitishwa kingono kama vile UKIMWI, maradhi ya zinaa, malengelenge na kisonono.

“Ukiamua kufanya ngono, kinaonyesha jinsi upaswavyo kuchagua mwenzi mmoja tu wa maisha, na chashikilia utakatifu wa ndoa. Nimefurahia kwelikweli kutumia kitabu hiki. Kina matokeo juu ya maisha za wale wanaokitumia. Niliona kwamba idadi ya wanawake wachanga katika programu yetu waliokuwa wakishika mimba ilipungua sana baada ya wao kuonyeshwa kitabu hicho.”

Ikiwa ungependa kupokea nakala ya kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi au kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki