Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/8 uku. 31
  • Je! Mungu Huunga Mkono Upande Wowote Michezoni?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Mungu Huunga Mkono Upande Wowote Michezoni?
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Sala Katika Michezo—Je! Mungu Husikiliza?
    Amkeni!—1990
  • Je, Nijiunge na Michezo ya Timu?
    Amkeni!—1996
  • Michezo ya Timu—Je, Yanifaa?
    Amkeni!—1996
  • Kuweka Michezo Mahali Payo Panapofaa
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/8 uku. 31

Je! Mungu Huunga Mkono Upande Wowote Michezoni?

MKIMBIAJI mshindi apiga magoti na kufanya ishara ya maombi, akitoa shukrani kwa ajili ya ushindi wake. Na bado, ni lazima tudhanie kwamba baadhi ya wakimbiaji wale wengine katika shindano hilo walisali pia kwa Mungu ili wapate ushindi—na wakashindwa.

Wanandondi wawili wapiga magoti kwenye kona zinazokabiliana za jukwaa la ndondi kabla ya duru ya kwanza ya pigano lao. Wote wafanya ishara ya msalaba, aina ya sala ya ukimya kwa Mungu ili wapate ushindi. Kisha mmoja amdengua yule mwingine na kumshinda. Kwenye mapigano mengine, ni mpiganaji mmoja tu ambaye huenda akamwomba Mungu apate ushindi, lakini mara nyingi yeye ama hushinda ama hushindwa.

Katika michezo ya timu, vikundi vya wachezaji vyaweza kusali kabla ya mchezo, unapoendelea, au hata baada ya kumalizika kwa mchezo. Kwa kielelezo, katika sekunde za mwisho za kinyang’anyiro cha mpira wa American Super Bowl, mpiga mkwaju mmoja alijitayarisha kufunga bao la ushindi wa timu yake au la ushinde kama angekosea. Mchezaji huyo alisema hivi baadaye: “Nilikuwa nikisali juu yalo.” Lakini baadhi ya wale walio katika timu ya upinzani walikuwa wakisali pia juu yalo—ili asifunge bao hilo.

Ingawa huenda pande zote mbili zikasali, ni lazima upande mmoja ushindwe. Hata timu yenye ushindi ambayo wachezaji wayo walisali wapate ushindi inaweza kushindwa katika mchezo unaofuata. Kwa kweli hatimaye, kufikia mwisho wa msimu wa michezo, ni lazima timu zile nyingine zote zishindwe, kwani kwaweza kuwa na mshindi mmoja tu katika ligi. Na bado, timu hizo nyingi zilizoshindwa zilikuwa na wachezaji waliosali wapate kushinda.

Katika makala moja yenye kichwa “Acheni Kutoa Sala, Tafadhali,” mwandishi wa michezo aliandika hivi: “Kwa sababu tu una madaha mengi juu ya vile ulivyo na uhusiano mzuri na Mungu, haimaanishi kwamba hiyo ni kweli. . . . Katika Vita ya Ulimwengu 2, askari-jeshi wa Ujerumani walikuwa na maneno yaliyoandikwa kwenye mishipi yao: Gott mit uns. Tafsiri: ‘Mungu yu pamoja nasi.’” Mwandikaji mwingine wa michezo alionelea hivi: “Mungu haungi mkono upande wowote katika michezo ya kandanda. Mambo ya kilimwengu kama hayo huamuliwa na wanaume na wanawake, si na yule Mweza Yote.”

Mtume Petro aliandika hivi: “Mungu hana upendeleo; bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki [kufuatia uadilifu, NW] hukubaliwa na yeye.” Kushiriki katika michezo yenye jeuri si “kufuatia uadilifu.” (Matendo 10:34, 35; Warumi 14:19) Kama Mungu angesikiliza sala za wale wanaomwomba wapate ushindi na mchezaji mmoja aumie au kuuawa, je, Mungu angelaumika?

Neno la Mungu lasema: “Tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.” (1 Yohana 5:14) Ili sala zijibiwe, ni lazima mtu ajue mapenzi ya Mungu na makusudi yake, na matendo ya mtu lazima yapatane na hayo.—Linganisha Mathayo 6:9, 10.

La, mapenzi ya Mungu na makusudi yake hayahusiani na michezo. Hivyo, wakati sala za kupata ushindi zinapotolewa huko, je, Mungu husikiliza? Kwa kweli, la.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

UPI/Bettmann

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki