Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 3/22 uku. 31
  • Ndege-Mpiga-Mbizi Mbeja

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndege-Mpiga-Mbizi Mbeja
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Cock-of-the-Rock—Mrembo wa Msitu wa Amazon
    Amkeni!—1998
  • Mchekeshaji Mwenye Manyoya wa Ziwa Viktoria
    Amkeni!—1993
  • “Mkazi wa Msituni Mwenye Kuvutia Kuliko Wote”
    Amkeni!—2000
  • Mwamba Mkubwa Ajabu
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 3/22 uku. 31

Ndege-Mpiga-Mbizi Mbeja

NENO “mbeja” laeleza ndege-mpiga-mbizi ifaavyo. Lamaanisha ‘kuwa safi na maridadi katika sura, chonjo na mchangamfu katika miendo na adabu.’ Hata hivyo, ikiwa wewe wapendelea zaidi neno la staha zaidi, waweza kutumia jina lake la Kilatini, Cinclus c. gularis.[1]

Kwanza niliona ndege-mpiga-mbizi huyo ametua juu ya mwamba mkubwa katikati ya kijito chenye kutiririka mbio kaskazini mwa Uingereza. Alikuwa na urefu wa sentimeta 18 tu, kutoka ncha ya mdomo wake hadi ncha ya mkia.[1a] Huyo ndege-mpiga-mbizi alikuwa na sura ya manyoya ya kahawia nyeusi iliyo safi kabisa, akiwa na kiduara safi cheupe kifuani kama kwamba ni cha kumkinga asijichafue kifua anapokula, kikianzia palepale chini ya mdomo hadi nusu ya kifua chake, kikionekana wazi sana kwa kutofautiana na vijanijani vibichi vyenye kuifunika miamba.[1b]

Akipuuza ule mngurumo na marasharasha ya poromoko la maji hapo karibu, huyo ndege alisimama kama kwamba miguu yake imebanwa imara mahali pamoja kwa bawaba za kumsaidia asianguke, huku akiinamisha kichwa chake na kuinama kwa uungwana, akitenda sawasawa na jina lake. Kwa ghafula akajitumbukiza ndani ya kile kijito na kupiga mbizi hadi chini kama kwamba kwa kupuruka. Halafu akatembea kupanda juu ya maji, akitafuta chakula cha mabuu ya inzi aina ya kadisi, mbawakavu wa majini, wadudu wapiga-makafi wa majini, buibui, viluwiluwi na tunutu wa majini wenye mikia mirefu au kereng’ende, na samaki wadogo nyakati fulani.[2] Wakati ndege-mpiga-mbizi anapofanya hivyo, macho yake hulindwa na ukope wa tatu. Huyo ndege awapo katika nchi-kavu, nyakati fulani ukope huo waweza kuonwa ukipepesa juu ya jicho, hiyo ikitoa wazo la kwamba ndege huyo anakonyeza macho.[3]

Mwinamo wa mgongo wa ndege-mpiga-mbizi umeundwa kwa njia ya kwamba nguvu ya maji yenye kutiririka mbio huweka kichwa chake chini. Pia yeye hutumia mabawa yake kusaidia kuzuia ile hali yake ya asili ya mwili kuelea juu ya maji. Mara kwa mara, yeye hupanda juu apate hewa na kuelea juu ya maji, au huenda akachagua kuogelea, ingawa hana miguu yenye utando.[4] Wakati atokeapo tena ili kurudi kwenye mwamba wake, yeye huwa safi kabisa sawasawa na alivyokuwa alipoingia kijitoni kwanza!

Yule ndege-mpiga-mbizi niliyekuwa nikimwangalia yaonekana alikuwa amemaliza pata-shika yake ya kutafuta chakula na kurudi kulisha makinda yake. Yeye hutengeneza kiota cha vijanijani vya miambani kilicho kama kuba, kilichofumwa kwa kambakamba za nyasi kavu juu ya mwamba, chini ya mizizi ya miti na vidato vya mwamba au kikiwa kimeingizwa chini ya kangaga zenye kuning’inia. Lakini hicho kiota huwa kimefichika vizuri sana kulingana na rangi ya mazingira hivi kwamba yawezekana usimame ukiwa chini yacho na using’amue kwamba kipo.[6] Mimi nilikuwa nimetafuta kiota cha ndege huyo kwa kitambo lakini wapi.

Halafu, nilipoendelea kutazama, kufumba na kufumbua ndege-mpiga-mbizi ndiye huyo-o kapuruka moja kwa moja kuingia katika lile poromoko la maji! Niliambaa polepole kwenye ukingo wa kile kijito ili nione nyuma ya lile poromoko la maji. Kiota chake kilijengwa ndani ya ufa juu ya mwamba nyuma ya lile anguko la maji. [7] Inasisimua kama nini kuona ndege huyo akiruka kwa kukatiza ndani ya maji ili kulisha makinda yake!

Siku hiyo ndege-mpiga-mbizi huyo mdogo aliye mbeja alinipa raha istahiliyo kukumbukwa.—Imechangwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki