Kweli Huyu Ni Chiriku?
CHIRIKU wajulikana ulimwenguni pote. Wao huishi katika kontinenti zote ila Antarktika iliyo baridi mno. Hata visiwa vingi vya bahari kuu vina chiriku kadhaa.[1] Na kwa kawaida wao huvutia sana. Kwa kielelezo wafikirie chiriku-dhahabu wa Amerika. Wao “huongezea nchi tambarare uchangamshi kwa urangirangi wao mwangavu, wa manjano na mweusi . . . , mirukoruko yao ya kupinduka na kuteremka kama kwamba wako juu ya vilima na mabonde yasiyoonekana hewani, na milio ya twitwitwi!”—Book of North American Birds.[2]
Hata hivyo, kuna chiriku mmoja awazidiye wote kwa uzuri wa kutazamisha—mnana-chiriku-Gouldi mwenye urefu wa sentimeta mbili, apatikanaye kaskazini mwa Australia, hasa katika mbuga za miti ya yukalipti. Huenda ukapata ndege aliyetekwa katika vizimba vya nyuni nchini mwenu. Ensaiklopedia moja yataarifu: “Hii imechangia upungufu mkubwa miaka ya majuzi.”[3]
Chiriku wana midomo iliyoundwa kwa ndani kushika na kuambua mbegu. “Kila mbegu hupachikwa katika mkato maalumu kando ya kaakaa na kusagwa kwa kuinua utaya wa chini juu yayo. Kisha lile ganda huambuliwa kwa msaada wa ulimi, hivyo kufungulia kokwa, ambayo humezwa.” (Birds: Their Life, Their Ways, Their World) Hata hivyo, chiriku-Gouldi “badala ya kuchukua [mbegu] ardhini hujirusha kwa usanifu hadi kwenye masuke yenye mbegu, au huzidonoa mbegu akiwa amekwamilia kijitawi kilicho karibu.”—The Illustrated Encyclopedia of Birds.[4]
Ukipata kuona chiriku-Gouldi, jihisi umebarikiwa kuwa ulishuhudia kiumbe wa rangi maridadi katika ndege mdogo jinsi hiyo.
[Picha katika ukurasa wa 31]
Chiriku-dhahabu wa Amerika
[Picha katika ukurasa wa 31]
Chiriku-Gouldi