‘Mmoja wa Mizaha Mikubwa ya Historia’
“MIMI mwenyewe nasadiki kwamba nadharia ya mageuzi, hasa kwa kadiri ambavyo imetumiwa, itakuwa mmoja wa mizaha mikubwa katika vitabu vya historia wakati ujao. Vizazi vijavyo vitastaajabu kwamba dhana hafifu sana na ya kishakashaka hivyo ingeweza kukubaliwa kwa urahisi wa kushangaza kwa kadiri hiyo.” Hayo yalikuwa maneno ya mtangaza-habari na mwandikaji Mwingereza Malcolm Muggeridge (1903-90) katika mihadhara aliyoitoa katika Chuo Kikuu cha Waterloo, Ontario, Kanada. Aliongezea: “Nadhani nimewahi kuongea nanyi kwamba katika historia hiki ni kimojapo vizazi vyenye kuamini zaidi mambo hivihivi tu, nami ningehusisha mageuzi kuwa kielelezo.”[1]
Basi kwa nini wanasayansi wengi sana hukubali mageuzi? Swali hilo na mengine mengi yafikiriwa kirefu katika kile kitabu cha kurasa 254 Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Ikiwa ungependa kusoma kitabu hiki, jihisi huru kupashana habari na Mashahidi wa Yehova katika eneo lako, au uandikie anwani ya karibu zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.
Kazi ya elimu ya Kikristo ya Mashahidi wa Yehova hutegemezwa na misaada ya kujitolea kwa hiari.