Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/8 uku. 32
  • “Uvutaji Sigareti Wanuka”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Uvutaji Sigareti Wanuka”
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 1/8 uku. 32

“Uvutaji Sigareti Wanuka”

Katika miaka ya majuzi Idara ya Huduma za Afya California imefanya kampeni kali ya kuelimisha dhidi ya kuvuta sigareti. Ujumbe ni mfupi na wenye maneno ya wazi na umeonekana katika mabango taifani pote. Ni nini baadhi ya ujumbe huo? “Wavutaji sigareti ni waraibu. Kampuni za tumbaku ni za uchuuzi. Uvutaji sigareti wanuka.” “Moshi kutoka kwa wavutaji mwaka huu utaua watu 50,000 wasio wavutaji. Uvutaji sigareti wanuka.” Chini ya pakiti ya sigareti, ujumbe mwingine wasema, “Nunua sasa. Lipa baadaye.” Ni wazi, ulipe kwa uhai wako. Ishara moja katika Kihispania yataarifu hivi: “Me muero por fumar.” Huo ni mchezo wa maneno uwezao kusomwa hivi, “Ninakufa kwa tamaa ya uvutaji sigareti” au, “Ninakufa kwa sababu ya uvutaji sigareti.” Ile picha ya nusu-fuvu-nusu-uso huelewesha wazi wazo hilo.

Mbinu tofauti itumiwayo katika nchi fulani-fulani kushawishi watu wasianze kutumia tumbaku na nikotini ni aina ya sigareti iitwayo “Kifo.” Pakiti nyeusi hiyo ina umbo la fuvu na mifupa iliyokingamana na ujumbe utaarifuo hivi: “Sigareti zina uraibu na hudhoofisha. Ikiwa wewe huvuti sigareti, usianze. Ikiwa wewe huvuta, acha.”

Ni vigumu kujua mbinu nyinginezo za tisho la mabango zina tokeo lolote juu ya wale ambao tayari ni wavutaji sigareti. Ingawa hivyo, muda wa miaka sita iliyopita “utumizi wa tumbaku katika California umeshuka sana kwa asilimia 27, karibu mara tatu kuliko wastani wa kitaifa.” (The Washington Post National Weekly Edition) Kampeni ya utangazaji wa mabango huenda ikawageuza hata wale wawezao kuanza kuwa wavutaji sigareti wajiepushe na zoea hatari hili. Hakika wale wadaio kuwa Wakristo wapaswa kuepuka uovu huu usio safi, wa ubinafsi. Mtume Paulo aliandika hivi: “Kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.”—2 Wakorintho 7:1.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki