Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/22 uku. 32
  • Msaada Wenye Thamani kwa Miradi ya Shuleni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msaada Wenye Thamani kwa Miradi ya Shuleni
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 2/22 uku. 32

Msaada Wenye Thamani kwa Miradi ya Shuleni

“MAJARIDA ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa kweli ndiyo yenye kuelewesha zaidi, yaliyo rahisi zaidi kusoma na kufahamu, ya wakati ufaao zaidi, majarida yatiayo moyo zaidi ambayo nimepata kusoma,” akaandika msomaji mmoja tineja. “Habari ya nyingi za miradi yangu ya shuleni imetoka kwa magazeti haya. Ninaposoma jambo fulani shuleni, makala kuhusu habari hiyo ipo ili kunitia moyo na kunisaidia kufahamu kichwa na umuhimu wacho.

“Kwa kielelezo,” msichana huyo akaelezea, “nilihitaji mada kwa ajili ya mradi wa sayansi kwa Maonyesho ya Sayansi tuliyohitajika kushiriki. Mradi huo ulihitaji vibandiko vitatu, ripoti, na kiolezo. Basi nilifikiria kukuza ile habari ya matokeo ya kuongezeka kwa joto duniani, iliyozungumziwa kwenye Amkeni!, Septemba 8, 1989 (Kiingereza). Nilitegemeza vibandiko vyangu kwa vielezi vilivyotokea kwenye makala na nikatumia habari iliyomo kwa ajili ya ripoti yangu. Mwalimu wangu wa biolojia alinipa A, na nilipata zawadi ya kwanza kwa upande wa ekolojia na uhifadhi-mazingira!”

Ikiwa ungependa kupata nakala ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! upelekewe kwa posta nyumbani kwako, au ikiwa ungependa kuwa na funzo la Biblia nyumbani bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki