Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kitendeshi cha Rh na Wewe
    Amkeni!—1994
  • Si Mwamba Wala Kisiwa Tena
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Itikio kwa Simulizi la Moja kwa Moja Asanteni sana kwa simulizi lenye kuhuzunisha sana la Larry Rubin, “Si Mwamba Wala Kisiwa Tena.” (Novemba 22, 1994) Wengi mara nyingi hukosa kufikiria wale ambao wameteseka katika wakati uliopita. Mwana wangu mwenyewe wakati fulani aliniambia kwamba ikiwa nilikuwa na imani kikweli, singehangaika! Lakini si kila mtu awezaye kusahaulia mbali tu yaliyopita. Tafadhali endeleeni kutokeza maono ya kibinadamu ya aina hii. Nasali kwamba jambo hili litalainisha mioyo fulani.

M. L., Uingereza

Ninatafuta maneno ya kueleza shukrani zangu. Mara nyingi sana sisi hukabili watu ambao wamepatwa na makovu kwa sababu ya kutendwa vibaya kwa wakati uliopita. Kuwasaidia kuwa na utendaji ndani ya kutaniko na kusitawisha uhusiano pamoja na Yehova ni kazi kubwa mno. Hiyo makala ilionyesha kwamba inawezekana kwa watu kama hao kujifunza kuhisi upendo na tumaini.

J. D., Kanada

Nimekuwa Mkristo kwa miaka 25 sasa. Nimemtumikia Mungu kwa uaminifu kwa akili yangu, lakini moyo wangu umehisi kana kwamba ulikuwa umefanyizwa kwa jiwe. Nilikulia katika familia ya uraibu wa alkoholi na kuteseka kwa mipigo, kutendwa vibaya kingono, na maumivu mengine. Yehova amenifanyia mengi, lakini sihisi upendo kwake. Simulizi la Larry Rubin lilinipa tumaini dogo kwamba huenda, huenda tu, siku moja nitaweza kulia kuhusu wakati wangu uliopita na kuwa na hisia. Huenda nitapata kile Larry Rubin alicho nacho sasa—upendo, tumaini, na ukubali.

A. F., Marekani

Masimulizi ya maisha yaliyotangulia yamekuwa kuhusu watu ambao walionekana kuwa watu wasio wa kawaida—wasiohofu, wasio na mafarakano ya kindani, wasio na udhaifu. Simulizi la Larry Rubin lilisimuliwa kutoka mwono tofauti. Yeye alikuwa mwenye kueleza mambo wazi na kufunua hisia zake za ndani. Masimulizi ya maisha ya aina hii ni halisi kwetu kwa sababu yanahusu mambo yanayotukia katika maisha zetu wenyewe.

F. D. S., Brazili

Kitendeshi cha Rh Kwa kweli ni jambo lenye kusifika jinsi Amkeni! hushughulikia mada zenye kubishaniwa kama hiyo. Katika makala “Kitendeshi cha Rh na Wewe” (Desemba 8, 1994), mfikio uliotumiwa si ule wa washupavu wa kidini. Hiyo mada ilishughulikiwa kwa usahihi wa kisayansi, kwa kutumia istilahi ya kitiba ya karibuni zaidi, na bado katika mitajo yaliyokuwa wazi na yenye kueleweka. Inathibitisha kuwa uwongo lile shtaka la kwamba Mashahidi wa Yehova ni washupavu wenye kushikilia maoni yao tu ambao hawaweki thamani kwenye uhai wa kibinadamu.

I. R., Ujerumani

Mimi ni mjamzito, na daktari wangu aliniambia nilihitaji sindano ya kunizuia kutengeneza zindiko dhidi ya damu ya mtoto wangu. Sikujua chochote kuhusu kitendeshi cha Rh na sikupinga. Nilipojua baadaye kwamba hiyo sindano inafanyizwa kutokana na damu, niliogopa kwamba huenda ikawa niliasi sheria ya Mungu juu ya damu. Makala yenu ilinisaidia kwa kueleza kwamba kupata hiyo sindano kwa msingi ni swala la dhamiri.

C. W., Marekani

Kuzungumzia Dini Ingawa nililelewa nikiwa Mkristo, nina haya sana kuhusu kushiriki kikamili katika kazi ya kuhubiri hadharani, hasa miongoni mwa wanashule wenzangu. Shauri mlilotoa katika makala “Vijana Huuliza . . . . Kwa Nini Kuongea Kuhusu Mungu?” (Septemba 22, 1994) lilinikumbusha umuhimu wa kazi hiyo. Nitakumbuka na kufanyia kazi kitia-moyo chenu ili niwe mwenye kustahili vya kutosha nikiwa mwalimu wa Neno la Mungu.

K. K., Nigeria

Nina umri wa miaka 12, na nimekuwa nikiaibika kwelikweli kusema mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Nilikuwa nikitamani wanafunzi wenzangu wasinione katika utumishi wa shambani. Hiyo makala ilinisaidia kuona kwamba si mimi peke yangu niliyelazimika kukabili tatizo hili, na ilinisaidia kushinda hisia hizi za aibu.

M. V. S., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki