Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 10/8 kur. 20-21
  • Tunda la Kimataifa Lenye Kupendeza Mno

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tunda la Kimataifa Lenye Kupendeza Mno
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Nanasi na Mmea Walo
  • Hilo Hulimwaje?
  • Upendezi Halisi
  • ‘Fulizeni Kuzaa Matunda Mengi’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Ndizi—Tunda la Ajabu
    Amkeni!—1994
  • Kupanda Mazao Kwenye Msitu wa Amazon
    Amkeni!—2000
  • Yehova Anawapenda Wale ‘Wanaozaa Matunda kwa Uvumilivu’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2018
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 10/8 kur. 20-21

Tunda la Kimataifa Lenye Kupendeza Mno

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA MEXICO

CHRISTOPHER COLUMBUS na kikundi chake yaelekea walikuwa ndio Wanaulaya wa kwanza kulionja wakati wa uvinjari wao wa West Indies katika 1493. Lilipelekwa kwa mfalme wa Hispania, naye pia alipendezwa na ladha yalo. Mabaharia walilifanya kuwa maarufu kote katika Amerika na, katika 1548, walilichukua hadi Visiwa vya Filipino ili kukuzwa.

Hatimaye, yapata 1555, tunda hili lenye kupendeza lilisafiri hadi Ufaransa. Kufikia miaka ya 1700, tayari lilikuwa likiandaliwa katika meza za baadhi ya wafalme wa Ulaya kwa fahari likiwa tunda la matajiri. Likaja kuwa maarufu hivi kwamba lilienea kote Ulaya na hadi Asia na Afrika. Kwa sasa, lavunwa hasa katika Brazili, Hawaii, Mexico, Filipino, Thailand, na nchi nyinginezo chache zenye tabia ya nchi ifaayo na udongo.

Hivyo baada ya karne tano za kusafiri, limefika maeneo ya mbali sana kutoka Amerika, na maeneo yalo menyeji. Je, unajua tunda tunalozungumza kulihusu? Ni lile nanasi lenye kupendeza mno.

Katika Mexico liliitwa matzatli, katika Karibea ananá, na katika Amerika ya Kati na Kusini nana. Yaonekana kwamba Wahispania ndio waliliita piña kwa sababu ya mfanano walo (wa koni) tunda la msonabari. Leo katika Kihispania lajulikana kuwa piña ama ananás, huku katika Kiswahili likijulikana kuwa nanasi. Hata jina lalo liwe lipi, wale ambao wamelionja wakubali kwamba lapendeza kinywani.

Nanasi na Mmea Walo

Nanasi lafananaje? Lina umbo la mviringo wa yai na huchipuka kitovuni mwa huo mmea. Hilo tunda lafunikwa na ganda gumu, na juu, kuna taji lililofanyizwa na majani mengi madogo ya rangi ya kijani kibichi, yenye ugumu wa kadiri. Mmea wa nanasi wenyewe una majani marefu, yaumbikayo kama kisu yanayokua kuelekea pande mbalimbali kutoka shinani. Huo mmea hukua kufikia kimo cha sentimeta 60 hadi 90, na hilo tunda laweza kuwa na uzani wa kilo mbili hadi nne.

Linapokuwa bado ndogo, hilo lafanana na tunda la msonabari, na ngozi yalo hubaki rangi ya zambarau. Hilo huwa rangi ya kijani kibichi linapokomaa, na kwa kawaida hugeuka kuwa rangi ya manjano-kijani-kibichi, kijani-kibichi-machungwa, ama jekundu hivi linapoiva. Wakati nyama yenyewe inapoiva, ina ladha tamu—yenye harufu nzuri na umajimaji.

Hilo Hulimwaje?

Unalimaje nanasi? Kwanza kabisa, ule udongo upatikanao katika maeneo ya tropiki wahitajiwa—wenye changarawe, wenye mboji nyingi, asidi, na madini yenye umunyu mchache, wenye kiwango cha juu cha unyevu. Kisha, ni muhimu kupanda moja ya chipukizi ndogo ambazo huchipuka kuzunguka sehemu ya chini ya hilo tunda na baki la mmea baada ya hilo tunda kuvunwa. Ama hilo taji la nanasi lenyewe laweza kukatwa na kupandwa. Hata hivyo, mmoja lazima angojee ili aweze kufurahia mazao yao, kwani huchukua zaidi ya mwaka ili ukomae na kutokeza mavuno.

Antonio, ambaye amekuwa akifanya kazi ya ulimaji wa mananasi kwa zaidi ya miaka 25, aeleza ufundi fulani ambao hutumiwa: “Ni muhimu kuweka kiwango kidogo cha calcium carbide kwenye kitovu cha huo mmea kabla ya hilo tunda kuanza kukua. Hili hufanywa ili kwamba mananasi yote yaweze kuvunwa kwa wakati mmoja, kwani yakiachwa yakue kiasili, mengine yatakua kwa kasi kupita mengine na uvunaji utakuwa mgumu zaidi.”

Nanasi linapokomaa lakini bado kuiva, lazima lifunikwe ili kulizuia lisichomwe na jua. Hilo hufunikwa kwa karatasi ama kwa majani ya mmea huohuo. Baada ya wakati wa kuiva kutimia, nanasi linakuwa tayari kuvunwa. Ambua hilo ganda kwa kisu, nawe ulifurahie likiwa vipande-vipande! Lakini uwe macho. Kula sehemu ya kati ya tunda kwaweza kutokeza mwasho ulimini. Hiyo ndiyo sababu watu wengine hula nyama yalo tu na kutupa sehemu ya kati.

Ukitaka kuonja nanasi lenye utamu na umajimaji, usivutiwe na sura yalo. Huku akituonyesha moja yalo, Antonio aeleza: “Watu wengine huchagua nanasi kwa maganda yalo, kama yako rangi ya kijani kibichi ama manjano. Lakini tunda laweza kuwa limeiva hata ikiwa ganda lalo ni lenye rangi ya kijani kibichi. Unapaswa kuligonga na vidole vyako. Likitoa sauti kana kwamba ni lenye shimo, ama mwanya, nyama yalo itakuwa nyeupe na ladha yalo itakuwa chachu. Lakini likitokeza sauti thabiti, kana kwamba limejaa maji, hapo liko tayari kuliwa—tamu na lenye umajimaji.” Kuna aina kadhaa ya tunda hili, lakini aina iliyo maarufu zaidi inaitwa Cayenne laini (Cayena).

Upendezi Halisi

Licha ya kufurahia hiyo ladha yenye kupendeza ya umajimaji ama vipande vya hilo tunda, unaweza kulifurahia likiwa kimiminiko fulani, ambacho chapatikana kikiwa mikebeni katika nchi nyingine. Pia, nanasi lina virutubisho vingine kama vile kabohidrati, utembo, vitamini, hasa A na C.

Katika Mexico unaweza kufurahia kinywaji chenye kuburudisha kilichotengenezwa kutokana na maganda ya nanasi. Ili kujitengenezea, weka hayo maganda katika kiwekeo pamoja na maji na sukari kwa siku mbili ama tatu. Mara kinapochachuka, unaweza kukiandaa kikiwa kinywaji cha baridi pamoja na barafu. Ni kinywaji chenye kuburudisha mno kiitwacho tepache na kina ladha yenye utamu wenye kuchachuka. Je, ungependa kupata bilauri moja? Katika Filipino, nanasi hulimwa ili kupata nyuzi kutoka kwa majani yalo. Hizi hutumiwa kutengeneza kitambaa chenye weupe uliofifia, changavu, na kizuri sana. Hicho hutumiwa kutengeneza vitambaa vya mikono, taulo, mishipi, shati, na marinda ya watoto na wanawake.

Katika karne chache zilizopita, nanasi limepelekwa nje hadi nchi nyingi ambazo halikuzwi. Wote wanaofurahia ladha yalo watumaini kwamba litaendelea na safari yalo kuzunguka ulimwengu, likiwapendeza wanadamu.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 20]

Juu: Nanasi. Century Dictionary

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki