Nyoka Mla-Panya—Aliumbwa kwa Ajili ya Kupanda
KITABU cha habari za nyoka katika Alabama chamfafanua nyoka mla-panya kuwa mpandaji mahiri. Huyu aonyesha ustadi wake kwa kupanda ile sehemu ya matofali ya jengo. Yaonekana yeye ni mdogo, kwani aweza kuingia vizuri katikati ya mianya ya matofali. Yeye hupenda kula panya-buku na panya wadogo.
The Audubon Society Encyclopedia of Animal Life yafunua ustadi wake maalumu wa kupanda hivi: “Nyoka wala-panya wana sehemu pana za chini ambazo ni legevu. Angalau kazi moja ya upana wa chini humwezesha kubeta kona kali na kujishikilia kwenye ganda na hivyo kuweza kumudu mwili. Huyo aweza kupanda mti mkubwa kwa kupenyezea mwili wake katikati ya vigongo vya ganda na kujivuruta juu angalau kwa sehemu akitumia sehemu pana ya chini.”
Kuwapo kwake kwenye mti kwaweza kumfanya awe shabaha ya makundi ya kunguru-samawati. Mpando wake mrefu kwenye upande wa jengo hili huenda hautaishia na mlo wa ndege au mayai ya ndege, bali waweza kuandaa lepe kwenye matofali yenye ujoto.