Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 12/8 uku. 32
  • ‘Lilijibu Maswali Yote’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Lilijibu Maswali Yote’
  • Amkeni!—1995
Amkeni!—1995
g95 12/8 uku. 32

‘Lilijibu Maswali Yote’

Akieleza kuhusu ule mfululizo katika Amkeni! la Februari 22, 1995, “Uelewevu Mzuri Zaidi wa Komahedhi,” msomaji mmoja kutoka Kentucky, Marekani, aliandika hivi: “Hivi majuzi nilihudhuria semina ya muda wa saa tatu juu ya habari hii. Ilipangwa na idara za elimu za hospitali kubwa mbili. Hiyo programu ilikuwa yenye kuelewesha, lakini nilijifunza mengi katika dakika 30 kwa kusoma Amkeni! kuliko nilivyojifunza kwa muda wa saa tatu kwenye semina (nalo halikugharimu dola 15).”

Msomaji mwingine wa Amkeni! alionelea hivi: “Nimesoma vitabu na makala kadhaa kuhusu komahedhi katika miaka mitatu iliyopita. Baadaye sikuzote nilikuwa na maswali ambayo hayakujibiwa. Makala zenu zilijibu maswali yangu yote kuhusiana na habari hii.”

Amkeni! huandaa habari ambayo husaidia wasomaji walo kukabili matatizo ya leo. La maana zaidi, hujenga tumaini katika ahadi ya Muumba ya ulimwengu mpya wenye amani. Ikiwa ungependa kujua mengi zaidi kuhusu itikadi na utendaji wa Mashahidi wa Yehova, watangazaji wa gazeti hili, tafadhali wasiliana nao kwenye Jumba la Ufalme la kwenu, au andikia anwani iliyo karibu nawe iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki