Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 6/22 uku. 17
  • Misiba ya Asili—Kumsaidia Mtoto Wako Kukabili Hali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Misiba ya Asili—Kumsaidia Mtoto Wako Kukabili Hali
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Gari Lako—Kimbilio au Mtego?
    Amkeni!—1995
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Msaidie Mtoto Wako Akabiliane na Huzuni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 6/22 uku. 17

Misiba ya Asili—Kumsaidia Mtoto Wako Kukabili Hali

MATETEMEKO ya dunia, chamchela, mioto, mafuriko, vimbunga—sisi ni hoi kama nini tunapokabiliwa na ghadhabu ya vitu vya asili! Watu wazima hupata kwamba inaweza kuchukua miaka mingi kabla ya picha za akilini zenye kuogofya zilizotokezwa na misiba ya asili kuanza kuondoka. Basi haishangazi kwamba watoto waweza kuhitaji msaada wa ziada ili wapate nafuu kutokana na mambo yaliyowapata.

Shirika la Serikali la Kushughulikia Hali ya Dharura la Marekani (FEMA) lasema kwamba mara tu baada ya msiba, kwa kawaida watoto huhofu kwamba (1) wataachwa peke yao, (2) watatenganishwa na familia, (3) jambo hilo litatukia tena, na (4) mtu fulani atajeruhiwa au kuuawa. Unaweza kufanya nini ukiwa mzazi ili kupunguza hangaiko la mtoto wako baada ya msiba kutukia? FEMA latoa mapendekezo haya.a

Jaribu kuweka familia pamoja. Kukaa pamoja huandaa uhakikishio kwa mtoto wako na kuondosha hofu yake ya kuachwa peke yake. Si vizuri kuacha watoto na watu wa ukoo au marafiki au kuwaacha katika kituo cha uhamiaji huku ukitafuta msaada. “Watoto hupata mahangaiko,” lasema FEMA, “nao watakuwa na wasiwasi kwamba wazazi wao hawatarudi.” Ikiwa ni lazima uende mahali, nenda na mtoto wako ikiwezekana. Kwa njia hiyo “mtoto [wako] hatakuwa na mwelekeo sana wa kukukwamia.”

Chukua wakati ili ueleze jinsi hali ilivyo kwa njia ya utulivu na kwa uthabiti. Mwambie mtoto wako kile unachojua kuhusu huo msiba. Ikihitajika, rudia maelezo yako mara kadhaa. Taja kitakachofuata kutendeka. Kwa kielelezo, unaweza kusema, ‘Usiku huu tutakaa pamoja katika mahali pa kimbilio.’ Sema na watoto wako kwa kimo chao, ukipiga magoti ikihitajika.

Mtie moyo mtoto wako azungumze. “Mawasiliano ni yenye msaada sana katika kupunguza hangaiko la mtoto,” FEMA lasema. Sikiliza kile ambacho kila mtoto akuambia kuhusu msiba na hofu zake. (Linganisha Yakobo 1:19.) Mwambie kwamba ni jambo la kawaida kuogopa. Mtoto wako akionekana kuwa mwenye kusita kusema, mwambie kwamba wewe unaogopa. Kufanya hivyo kwaweza kufanya iwe rahisi kwake kueleza hofu zake, hivyo kukipunguza hangaiko lake. (Linganisha Mithali 12:25.) “Ikiwezekana, tia ndani familia nzima katika mazungumzo.”

Husisha watoto katika utendaji wa usafi. Mnaposafisha na kurekebisha nyumba, wape watoto migawo yao wenyewe. “Kuwa na kazi fulani ya kufanya kutawasaidia waelewe kwamba mambo yote yatakuwa shwari.” Hata hivyo, mtoto mdogo huhitaji uangalifu wa kipekee. FEMA laeleza: “Mtoto kama huyo anaweza kuhitaji utunzi mwingi zaidi wa kimwili, kukumbatiwa zaidi; na hilo hufanya iwe vigumu zaidi kwa wazazi kushughulikia mambo mengine ambayo yanapaswa kufanywa. Kwa kusikitisha hakuna njia ya mkato. Mahitaji ya mtoto yasiposhughulikiwa, hilo tatizo litaendelea kwa muda mrefu zaidi.”

Jambo moja la mwisho lapaswa kukumbukwa. FEMA lashauri wazazi: “Hatimaye, wewe unapaswa kuamua ni nini kilicho bora zaidi kwa watoto wako.” Kutumia miongozo hiyo yaweza kukusaidia kukabili hali ngumu kwa njia bora zaidi.

[Maelezo ya Chini]

a Yametolewa katika vichapo Helping Children Cope With Disaster na Coping With Children’s Reactions to Hurricanes and Other Disasters, vilivyotangazwa na FEMA.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki