Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 7/8 uku. 31
  • Mistral—Mtengeneza-Mandhari Mwenye Ustadi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mistral—Mtengeneza-Mandhari Mwenye Ustadi
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1998
  • Kutumia Nguvu za Upepo
    Amkeni!—1995
  • Baada ya Dhoruba—Kutoa Misaada Huko Ufaransa
    Amkeni!—2000
  • “Miti ya Yehova Imeshiba”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 7/8 uku. 31

Mistral—Mtengeneza-Mandhari Mwenye Ustadi

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UFARANSA

VITALU sambamba katika safu zenye mpangilio mzuri, vijiji vikiwa vimejikusanya pamoja katika pande za vilima zisizo na upepo, na miti ionekanayo kuwa imepoteza majani na matawi yayo yote kwa upande mmoja. Hizo ni mandhari za kawaida za Provence katika kusini-mashariki mwa Ufaransa, na upepo uitwao mistral ulichangia yote hayo.

Upepo huo wa mistral ni wenye umashuhuri kama pepo nyinginezo mashuhuri, kama vile foehn wa Alps, pampero wa Amerika Kusini, chinook wa Rockies ya Amerika Kaskazini, harmattan wa Afrika kaskazini-magharibi, na ule Eurakilo, unaotajwa katika Biblia.a (Matendo 27:14) Jina mistral latokana na neno la Kiprovence limaanishalo “ustadi.” Kwa kupatana na jina lao, upepo huo waweza kuvuma kufikia mwendo wa kilometa 200 kwa saa.

Upepo huo wa mistral hutokana na “pambano” la daima kati ya msongo wa juu wa hewa juu ya Ufaransa ya kati na msongo wa chini juu ya Mediterenia. Nguvu yao nyingi yatokana na kile ambacho huitwa athari ya kipito cha mlima. Ukipitishwa kati ya milima Alps na uwanda wa juu wa Massif ya Kati, upepo wa mistral hufikia upeo wa nguvu zao baada ya kutoka bonde la Donzère, kana kwamba umemiminwa kupitia mpare.

Wakati wa kiangazi mistral hupeleka mbali mawingu. Wakati wa kipupwe, mistral hufanya baridi ionekane kuwa haiwezi kuvumilika, nao waweza kusababisha barafu ya baada ya kipupwe katika eneo ambalo ni la joto la kiasi. Katika majira yoyote ya mwaka mistral hulaumiwa kufanya wakazi wa huko kuwa watu wa kuchokozeka haraka.

Lakini ni katika misitu maridadi ya mierezi ya Lubéron ambamo mistral huonyesha kipawa chao kabisa, ukiunda miti hivi kwamba inafanana na bendera zenye kufuata upepo. Kwa upande mwingine, mara nyingi mistral huchochea mioto yenye kuchoma misitu wakati wa majira ya kiangazi, hivyo ukiharibu matunda ya kazi yao.

“Siku tatu, sita, au tisa,” ndivyo usemavyo msemo wa kale wa Kiprovence kuhusu ni muda gani mistral huvuma. Lakini upepo huu wenye ustadi waweza kuvuma kwa muda mrefu zaidi kuliko hizo siku. Kwa kielelezo, katika 1965 ulivuma kwa siku 23 bila kukoma!

Mwanadamu amejifunza namna ya kukabiliana na mistral. Vitalu sambamba hulinda mashamba, na nyumba za zamani za vijiji ni nadra sana ziwe na madirisha na milango kuelekea upande wa kaskazini. Ingawa pepo zao baridi zaweza kusumbua sana, hata hivyo mistral waweza kuonwa kuwa mtengeneza-mandhari mwenye ustadi.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa habari zaidi ona Insight on the Scriptures, Buku 1, ukurasa 770, kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki