USIHARIBU, NAWE HUTAKUWA NA UHITAJI
KATIKA jamii yetu ya kisasa ya watumizi, njia isiyodhuru ya kuondosha taka na vitokezwaji visivyotakikana imekuwa jambo lenye kuogofya. Kinyume na hilo, uumbaji wa Mungu ni ajabu ya utunzaji matumizi na uregeshaji. Kwa kielelezo, fikiria sega la asali. Nta ya nyuki, kifaa cha ujenzi wa sega la asali, ni bidhaa ghali sana—nyuki huhitaji gramu 16 za asali na kiwango kisichojulikana cha chavuo ili kutengeneza gramu 1 tu ya nta. Nyuki hawa hupangaje bajeti ya nta yao? “Kuta tatu za nta za vijumba vya sega la asali hukutana kwa pembe ya digrii 120, zikifanyiza safusafu za pembesita,” chaeleza kitabu By Nature’s Design. “Kigezo hiki huwezesha nyuki kupunguza kiwango cha nta wanayotumia, huku kikiandaa muundo thabiti ambao katika huo wanaweza kuhifadhi asali.” Kwa hiyo muundo wa kibusara huunganisha urembo wa umbo pamoja na ufanyaji kazi wenye kutunza matumizi, na sega hilo laweza kuregeshwa!
Ikiwa wewe hufurahia kusoma makala zihusuzo sayansi na maajabu ya asili na ungependa kupata Amkeni! kwa ukawaida, wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika ujirani wako au andika ukitumia anwani ya karibu zaidi kati ya zile zilizoorodheshwa kwenye ukurasa 5.