Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/8 kur. 17-18
  • Kuuvumbua Ulimwengu wa Miti Maridadi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuuvumbua Ulimwengu wa Miti Maridadi
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Umaridadi na Fahari
  • Shangwe za Kimsimu
  • Usimamizi wa Kisayansi
  • Vuli Ni Majira Yenye Kuvutia Sana
    Amkeni!—2001
  • Bustani za Japani—Mifano Midogo ya Asili
    Amkeni!—1993
  • “Miti ya Yehova Imeshiba”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Maua ya Mcheri Yenye Petali Zinazovutia Tangu Zamani
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/8 kur. 17-18

Kuuvumbua Ulimwengu wa Miti Maridadi

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UINGEREZA

WESTONBIRT, kijiji kimoja katika Cotswolds (safu ya milima) katika Uingereza, chajulikana sana kwa bustani-miti yacho. Ni mmojapo mikusanyo ya kale zaidi iliyo mikubwa zaidi na mizuri sana ya miti na vichaka ulimwenguni. Acheni tuutazame kwa ukaribu zaidi.

Umaridadi na Fahari

“Hakuna mtu asiyeguswa hisia na umaridadi, fahari na uzuri wa mkusanyo huu,” asema Hugh Angus, msimamizi wa bustani-miti hiyo. Na kwa kuamua kulingana na idadi ya wageni ambao hurudi tena na tena, yaelekea anasema kweli.

Bustani-miti hiyo ina miti na vichaka 18,000, ambavyo huwakilisha karibu nusu ya zile spishi na aina 9,000 ambazo hukua katika kanda zisizo na joto sana wala baridi sana. Wageni huruhusiwa kuzunguka-zunguka kwa uhuru katika hektari 240 za bustani hiyo, lakini ili kuwasaidia kufurahia zaidi, “tumegawanya bustani-miti katika sehemu nne na kudokeza wakati mzuri wa kuzuru kila sehemu,” kitabu rasmi cha uongozi chaeleza. Kwa kuongezea, kuna mandhari za kipekee, kama vile Kijia cha Rangi za Vuli, Mkusanyo wa Cheri wa Hillier, na Mkusanyo wa Spishi Zenyeji, zote zikiwa zimeonyeshwa kwa vibao vya ishara na ramani.

Shangwe za Kimsimu

Duru ya kimsimu ya Kizio cha Kaskazini ni shangwe ya kiasili. Katika bustani-miti hiyo, kila msimu una uvutio wao. Wakati wa kipupwe ndio wakati bora zaidi wa kuona unamna-namna mwingi wa mipia na kuona maumbo yenye madaha, miundo yenye kupendeza, na rangi zenye kushangaza za miti yenye kupukutisha majani. Baadaye, vichaka na miti ambayo huchanua wakati wa masika—azalea, camellia, cheri, magnolia, na rhododendron—hutoa wonyesho wayo wenye fahari, na utando wa maua-mwitu huongezea umaridadi wa mandhari hiyo.

Majani mengi matulivu yaweza kuonekana kwenye bustani-miti wakati wa kiangazi, kabla ya wonyesho wa mchanuo wa kibotania wa wakati wa vuli. Wageni wapatao 90,000 huja kwa wingi Westonbirt katika Oktoba ili kuona tamasha hii, ambayo ina sifa sana. Hapa aina nyingi za miti aina ya maple ya Kijapani, ikiwa na rangi yayo nyekundu iliyokolea, ndiyo huvutia zaidi.

Violezo vingi vya kale vya maple ya Kijapani huku Westonbirt huenda vikawa miti ya awali iliyoletwa katika kipindi cha Edo, 1603-1867. Kwa kuhuzunisha, hakuna rekodi za majina ya Kijapani kwa aina hizi za kale. Miti ya maple ilikuja kupoteza umashuhuri katika Japani baada tu ya kupelekwa Ulaya, kwa hiyo miti hii ya awali iliyopo haiwezi kuchunguzwa kwa kulinganishwa na mikusanyo au miti iliyopo katika nasari ya Kijapani. Miti ya kale ya maple ya Kijapani inapokwisha, mingine michanga inapandwa. Karibu kila mti una jani la umbo na rangi tofauti. Miti hiyo ilikuzwa kutoka mbegu zilizokusanywa kutoka miti ya maple ya kale, na kuteuliwa kwa sababu ya rangi zayo za wakati wa vuli. Ili kuandaa ulinzi na kivuli, miti hiyo ya maple hupandwa miongoni mwa miti mipevu ya oki na mipia. Hii pia huandaa mandhari-nyuma ya rangi za dhahabu na kijani ambazo kupitia kwazo miali ya nuru ya jua la wakati wa vuli huangaza miti hiyo ya maple.

Usimamizi wa Kisayansi

Bustani-miti ya Westonbirt ilianzishwa ikiwa hobi ya kibinafsi katika 1829 na kuchukuliwa na Tume ya Uingereza ya Misitu katika 1956. Lengo si kuandaa tafrija kwa umma tu. Kwa kweli, lengo kuu ni kusitawisha mkusanyo wa kisayansi unaofaana sana na hali za mahali mbalimbali. Kwa kusudi hili, utafiti unafanywa kuhusiana na namna za msambazo, na matokeo—mafanikio na ukosefu wa mafanikio—hushirikiwa na bustani nyinginezo za botania.

Westonbirt imeanzisha mfumo wa orodha wa kikompyuta ambao hurekodi habari kuhusu kila kiolezo—kilipotoka, maendeleo tangu mbegu hadi upevuko, afya na matibabu yoyote ya maradhi, na hata kisababishi cha kifo. Kazi nyingine muhimu ni msambazo wa spishi nadra au zisizo za kawaida, kutia ndani zile zilizoorodheshwa na Muungano wa Kuhifadhi Maumbile ya Asili na Rasilimali Asilia, zilizohatarishwa katika mazingira yazo ya kiasili. Mbegu hupatikana kutoka vyanzo vilivyohakikishwa ili kuepuka utokezaji wa mivyauso, na violezo hupelekwa kwa bustani-miti.

Westonbirt ni kitovu cha elimu pia. Kuna programu juu ya utambulishaji wa miti, hotuba juu ya ukataji miti, ziara za mihadhara, na maonyesho ya slaidi. Katika nyakati fulani za mwaka, mazungumzo yenye picha huandaliwa kila siku kwa watoto wa shule wanaozuru.

Tunapokuwa tukiondoka bustani-miti kwa kusita, tukiwa tumefurahishwa sana na ono hilo lisilosahaulika, twahisi msukumo wa kurudi na kushiriki fahari za misimu mingineyo. Kuvumbua ulimwengu huu maridadi wa miti kumetupatia utambuzi mwingi wa fahari yayo na vilevile umaana wayo katika namna ya maisha ya dunia.

[Picha katika ukurasa wa 17]

Juu: Mteashuri wa Lawson

Katikati: “Maple” wa Kijapani

Chini: Mwerezi wa Lebanoni

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki