Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/8 uku. 32
  • Wakati Ujao Mzuri Ajabu kwa Sayari Dunia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Ujao Mzuri Ajabu kwa Sayari Dunia
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 9/8 uku. 32

Wakati Ujao Mzuri Ajabu kwa Sayari Dunia

“UTAFITI waonyesha kwamba Dunia sasa imepatwa na joto jingi mno kuliko ambavyo imekuwa kwa miaka 600,” laripoti gazeti la Toronto Globe and Mail. Katika 1995 kipindi cha joto kali lisilo la kawaida katika Marekani ya kati kilisababisha vifo vya zaidi ya watu 500 Chicago. Hali kama hizo zenye kupita kiasi zilipata India na Australia, huku Uingereza ikikumbwa na “kiangazi kikavu kupita vyote katika miaka 200.”

Kisababishi cha hilo ni nini? Henry Hengeveld, mtaalamu wa tabia-nchi anayefanya kazi na Idara ya Mazingira ya serikali katika Kanada, asema hivi: “Uthibitisho mwingi wadokeza kwamba kuna uvutano wa kibinadamu ulio wazi juu ya tabia-nchi ya duniani pote.” Kulingana na ripoti ya Globe and Mail, “halihewa isiyo ya kawaida inapatana na mifano ya dunia inayoongozwa na kompyuta inayoigiza athari za kuongezeka kwa joto duniani, kunakofikiriwa husababishwa na kuchomwa kwa fueli za visukuku.”

Kuongezeka kwa joto duniani bado kwajadiliwa katika nyanja za kisayansi. Hata hivyo, The New Encyclopædia Britannica yataja: “Jamii ya kibinadamu inatumia vibaya mazingira ya anga-hewa haraka zaidi kuliko inavyoweza kujifunza kuihusu.”

Kwa kufurahisha, Biblia hutuambia kwamba dunia “hudumu daima.” (Mhubiri 1:4) Hiyo ni kwa sababu Muumba, Yehova Mungu, hatamruhusu mwanadamu au kani zozote za kiasili ziiharibu. Kinyume cha hilo, yeye ‘atawaharibu hao waiharibuo [dunia].’—Ufunuo 11:17, 18.

Kwa kuongezea, Biblia hutuhakikishia kwamba Yehova Mungu ametayarisha wakati ujao mzuri ajabu kwa sayari yetu, Dunia, na kwa wanadamu wote watiifu. “Wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa amani.” Twaweza kuwa na furaha kama nini kwamba wakati ujao wa dunia umo mikononi mwa Mungu, si mikononi mwa mwanadamu!—Zaburi 37:11; 72:16; Isaya 65:17-25; 2 Petro 3:13.

Ikiwa ungependa kupata nakala za wakati ujao za Amkeni!, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lako au andika kwa kutumia anwani iliyo karibu nawe kati ya zilizoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Picha ya NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki