Ukurasa wa Pili
Kutoka Maneno Yaumizayo Hadi Maneno Yaponyayo 3-11
Maneno yenye kuudhi huharibu uhusiano kwa kadiri gani? Kwa nini watu wengine hushusha watu ambao wao hudai kuwapenda? Ni nini kiwezacho kufanywa ili kuondoa kabisa usemi wenye kuudhi katika maisha ya mtu?
Kweli Ilinirudishia Uhai Wangu 12
Alikuwa mraibu wa dawa za kulevya akiwa na umri wa miaka 14 naye alipambana na uraibu na mtamauko kwa miaka mingi. Jifunze jinsi kweli ya Biblia ilivyobadili maisha yake.
Sigareti—Je, Wewe Huzikataa? 21
Ingawa pindi moja kuvuta sigareti kulikuwa kunapendwa sana na kuonwa kuwa mamboleo, sasa kumeshambuliwa. Kwa nini kuvuta sigareti kunapaswa kukataliwe?