Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 11/22 uku. 32
  • Kitu Ambacho Vijana Huhitaji Leo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kitu Ambacho Vijana Huhitaji Leo
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 11/22 uku. 32

Kitu Ambacho Vijana Huhitaji Leo

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 14 wa New Jersey, Marekani, alisema kwamba mwanzoni mwa mwaka huu alipaswa kuandika ripoti juu ya “Kwa Nini Wanafunzi Huiba Mitihani.” Alipeleka shuleni kitabu chake Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi ili kufanya utafiti. Mmoja wa wanadarasa alikinyanyua na kuanza kusoma vichwa vya sehemu katika yaliyomo, kama vile “Ngono na Maadili,” na “Urafiki na Mtu wa Jinsia Tofauti, Upendo na Jinsia Tofauti.”

“Nichukue kitabu hiki?” mwanashule mwenzake aliuliza.

“Nilieleza kwamba hii ilikuwa nakala yangu,” huyu mwanafunzi akasema, “lakini nitamletea nakala yake. Nilipofanya hivyo, mwanadarasa mwingine alikiona kitabu hicho na aliniomba nimpe kimoja pia. Muda mfupi baadaye, nilileta vitabu kumi vya Vijana Huuliza kwa wanafunzi waliohitaji nakala.”

Huyo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14 ahisi kwamba kitabu hicho ni chenye thamani kuwa nacho. Alisema: “Kwa kweli twakihitaji kichapo hiki kwa sababu kuwa kijana siku hizi ni jambo gumu sana.”

Ikiwa ungependa kupata nakala ya kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi au ungependa mtu fulani akutembelee nyumbani kwako kuzungumza thamani ya elimu ya Biblia pamoja nawe, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ikufaayo zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki