Ukurasa wa Pili
Msitu wa Mvua wa Amazon—Hekaya na Uhalisi 3-13
Watengeneza-barabara, wakata-miti, wachimba-migodi, wafugaji, na wakulima wa kiwango kikubwa kila mwaka huharibu maelfu ya kilometa za mraba za msitu wa mvua wa Amazon. Asilimia inayokadiriwa kuwa 10 ya msitu huo huenda tayari imeharibiwa. Uharibifu huu unaoendelea utaathiri ulimwengu wote.
Mashahidi wa Yehova Watetewa Katika Ugiriki 14
Ni dini nyoofu iliyo mashuhuri, na washiriki wayo wamechangia sana hali-njema ya ujirani wao.
Kudhulumu—Kuna Ubaya Gani? 17
Ikiwa washawishiwa kudhulumu, kumbuka kwamba Mungu aliwaharibu wadhulumu wa kale walioitwa “Wanefili”!—Mwanzo 6:4-7.