Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 7/8 uku. 32
  • “Sikupenda Kamwe Kusoma Amkeni!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Sikupenda Kamwe Kusoma Amkeni!”
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 7/8 uku. 32

“Sikupenda Kamwe Kusoma Amkeni!”

Hayo ni maneno ya mwanafunzi mmoja kwenye San Jose State University, California, ambaye anachukua mtaala wa Mafunzo ya Mazingira. Yeye aendelea hivi: “Nilikuwa na wazo kwamba gazeti hilo lingenihubiria—‘Nenda kanisani’ au, ‘Kuwa Shahidi wa Yehova.’ Hata hivyo, niliposoma toleo hili (Januari 8, 1996, ‘Sayari Yetu Iliyotishwa—Je, Yaweza Kuokolewa?’), nilishangaa kwamba ilikuwa yenye kueleza mambo ya hakika sana! Makala hizo zatia ndani mchoro wenye kuarifu wa ‘Baadhi ya Matatizo Makuu ya Kimazingira ya Ulimwenguni,’ ambayo huonyesha mahali ambapo misitu hufyekwa, mahali penye taka zenye sumu, uchafuzi wa kiangahewa, uhaba wa maji, spishi zilizohatarishwa, na kudhoofika kwa ardhi.

“Hadi sasa sina watoto, lakini nikipata kuwa nao nina wasiwasi ikiwa watakuwa na hewa safi ya kupumua, bustani za kuchezea, au maji ya kuendelea kuishi. . . . Nawapongeza kwa makala hizo.”

Amkeni! sasa hugawanywa kwa nakala zipatazo milioni 18.3 kila toleo katika lugha 80, kati yazo 56 huchapishwa sawia. Ikiwa ungependa kusoma gazeti hili kwa ukawaida, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo unamoishi, kwa simu au kwenye Jumba la Ufalme la mahali ulipo, au uandike ukitumia anwani ihusuyo kati ya zilizoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki