Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/8 uku. 32
  • “Kilikuwa Kitabu cha Kwanza Alichopata Kusoma”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kilikuwa Kitabu cha Kwanza Alichopata Kusoma”
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 9/8 uku. 32

“Kilikuwa Kitabu cha Kwanza Alichopata Kusoma”

Mashahidi wa Yehova katika Ukrainia kwa kawaida huzungumza na watu wanaongojea magari-moshi. Mwanamke mmoja aliyeonyesha upendezi katika Biblia alipewa nakala ya Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, kichapo kitumiacho picha kwa wingi katika historia yake inayofuatana ya matukio ya Biblia.

Baadaye, katika stesheni hiyohiyo, mwanamke huyo akamwona yule Shahidi tena akamshukuru kwa kile kitabu, akieleza: “Mwanangu hakupenda kusoma vitabu vyake vya shule. Hakuwa akivisoma kamwe. Lakini nilipompa kitabu Hadithi za Biblia, aliziona picha akawa na msukumo wenye nguvu wa kukisoma. Alikisoma kitabu chote kwa karibu majuma mawili hivi. Kilikuwa kitabu cha kwanza alichopata kusoma. Lakini zaidi ya yote, alifurahi kupata kumjua Mungu. Na mimi mwenyewe nafurahi kuona mabadiliko anayofanya. Tafadhali nipe kitu kingine zaidi cha kusoma.”

Mwanamke mwingine alikuwa amesimama kando naye akasikia mazungumzo hayo. Aliomba ikiwa angepata nakala ya Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Wewe pia waweza kupata nakala ya kitabu hiki chenye kurasa 256 au mtu fulani akutembelee nyumbani kwako kuzungumza pamoja nawe manufaa za elimu ya Biblia, kwa kuandikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani iliyo karibu nawe zaidi iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki