Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/8 uku. 31
  • Mazoezi ya Mwili Yenye Kupita Kiasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazoezi ya Mwili Yenye Kupita Kiasi
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Kitakachonichochea Kufanya Mazoezi?
    Vijana Huuliza
  • Je, Unafanya Mazoezi ya Kutosha?
    Amkeni!—2005
  • Njia ya 3—Fanya Mazoezi
    Amkeni!—2011
  • Afya Njema—Waweza Kuifanyia Nini?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 9/8 uku. 31

Mazoezi ya Mwili Yenye Kupita Kiasi

“TOKEO lisilo la kawaida la harakati ya mazoezi ya mwili,” lasema gazeti The Toronto Star, ni “wafanya-mazoezi kupita kiasi wasioweza kujidhibiti.” Gazeti Star laripoti kwamba kufanya mazoezi kupita kiasi huwataabisha wanaume na wanawake. Wanaume waweza kufanya mazoezi kupita kiasi ili wapate tena nguvu za ujana, wasema madaktari na wanatiba fulani, lakini kwa kawaida sababu kuu za wanawake kufanya mazoezi kupita kiasi ni kudhani kwamba hawana umbo zuri na matatizo ya ulaji.

Wengi huanza kufanya mazoezi ili wahisi na kuonekana vizuri zaidi lakini hatimaye hufanya mazoezi kupita kiasi. Richard Suinn, mwanasaikolojia wa michezo aliye pia mshauri wa timu kadhaa za Olimpiki, adai kwamba kufanya mazoezi kupita kiasi hudhihirika “kunapotegemea uwajibikaji wa kihisia-moyo badala ya mazoezi sahili ya mwili.” Wanaposhughulikia tatizo hili, madaktari na wanatiba hujaribu kuhakikisha matokeo ya mazoezi kwa maisha ya wagonjwa. Ikiwa wana kazi-maisha yenye kudai mno na wanatunza nyumba na watoto, kufanya mazoezi kupita kiasi kutakuwa na matokeo yasiyofaa kwa hali-njema yao. Kulingana na Dakt. Thomas Schwenk, profesa wa tiba ya familia, “huenda wakawa wangali wenye afya kimwili, lakini wamevurugika kijamii, wamevurugika kikazi, na kukosa upatano katika familia.”

Gazeti Star laorodhesha ishara fulani za kuonya zinazohusiana na waraibu wa kufanya mazoezi: ‘Uteuzi wa mazoezi ya kufanywa ukiwa peke yako, kama vile kuendesha baiskeli, kuogelea, kukimbia au kuinua uzani; ukosefu wa kubadili ratiba za kufanya mazoezi; kuitikadi kwamba ni lazima kufanya mazoezi na kwamba kukosa kuyafanya hakuwezi kuvumilika; na kudhoofika kwa upande mwingine wa maisha ya kibinafsi.’

Ingawa watu wanaofanya kazi katika nyanja za mazoezi ya mwili hukiri manufaa za mazoezi ya kiasi, wao huonya pia kuhusu matokeo yenye kudhuru ya mazoezi ya kupita kiasi.—1 Timotheo 4:8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki