Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Yesu alihusika na shughulikio gani katika eneo la nyumbani kwake? (Marko 6:3)
2. Ni nani aliyekuwa Mkristo katika Roma ambaye Paulo alimpenda sana mama yake hata Paulo akamwita mama yake mwenyewe? (Waroma 16:13)
3. Katika Hebroni wapelelezi waliotumwa na Musa waliwaona watu gani ambao ukubwa wao usio wa kawaida uliwaogofya sana kumi kati yao hivi kwamba waliogopa kuingia katika Bara Lililoahidiwa? (Hesabu 13:22, 32, 33)
4. Kulingana na vipimo vya kale, ni kiasi gani cha mafuta ya zeituni yaliyotumiwa katika kutengeneza mafuta matakatifu ya kutia-mafuta? (Kutoka 30:24, NW)
5. Ni nini litakalopata “jina la mtu mwovu”? (Mithali 10:7)
6. Ni mahali gani ambapo msafara wa waombolezaji wa Yakobo ulitua ili waomboleze kwa siku saba kabla ya yeye kuzikwa katika pango la Makpela? (Mwanzo 50:10)
7. Ni kwa nini Mfalme Ahasuero wa Uajemi aliamuru maofisa wa makao yake wamlete Malkia Vashti mbele yake? (Esta 1:10, 11)
8. Ni tukio jipi lililoongoza kwenye kifo cha Absalomu? (2 Samweli 18:9)
9. Kalebu alitoa zawadi gani kwa mtu yeyote ambaye angetwaa ngome ya Debiri? (Yoshua 15:16)
10. Akionyesha kudumu kwake milele, Yehova ajifafanua akitumia maneno gani katika kitabu cha Ufunuo? (Ufunuo 1:8; 21:6)
11. Ni nini lililokuwa vazi la kidesturi la kuombolezea katika nyakati za Biblia? (Mwanzo 37:34)
12. Akikataa mwaliko wa Daudi, Barzilai alipendekeza nani atwae mahali pake katika makao ya kifalme? (2 Samweli 19:37)
13. Ni kwa kufunua nini Paulo aliponea kupigwa mijeledi alipokuwa Yerusalemu? (Matendo 22:24-29)
14. Ni wapi Mfalme Sauli alimwendea mwasiliani-roho? (1 Samweli 28:7)
15. Kwa kumdhihaki, Waroma walikiweka nini kwenye mkono wa kulia wa Yesu na baadaye kukitumia kumpiga kichwani? (Mathayo 27:29, 30)
16. Ni nani ambaye zamani alikuwa malaya aliyekuja kuwa nyanya wa kale wa Yesu? (Mathayo 1:5)
17. Ni kupitia jiwe jipi lenye makali mke wa Musa, Sipora, alimtahiri mwana wake na hivyo kuepusha msiba? (Kutoka 4:25)
18. Ni kupitia nini watu waliofufuliwa watahukumiwa? (Ufunuo 20:12)
19. Ni nani ambaye jina lake lamaanisha “Mkinzani”? (Zekaria 3:1)
20. Shtaka dhidi ya “mwanamume mzee” halipasi kukubaliwa hadi lithibitishwe na nini? (1 Timotheo 5:19)
21. Ni nani aliyemkamata Yeremia kwa shtaka lisilo la kweli la kwamba alinuia kwenda kwa Wababiloni? (Yeremia 37:13, 14)
22. Kwa sababu ya dhambi ya Akani, Waisraeli walishindwa na wanaume wa jiji gani? (Yoshua 7:4, 5)
23. Mtu anayejiweza ambaye hataki kufanya kazi hapasi kuruhusiwa kufanya nini? (2 Wathesalonike 3:10)
24. Kwa sababu ya kuwa waovu, ni wana gani wawili wa Yuda waliouawa na Yehova? (Mwanzo 38:7-10)
25. Katika Israeli la kale kushindwa kushika nini kuliadhibiwa kwa kifo? (Kutoka 31:14, 15)
Majibu ya Maswali
1. Useremala
2. Rufo
3. Wana wa Anaki, ambao waliwadhania kuwa wazao wa Wanefili
4. Hini
5. Litaoza
6. Atadi
7. Ili aonyeshe uzuri wake
8. Alipokuwa amepanda nyumbu, kichwa chake kilinaswa na matawi ya mti mkubwa sana, yakimning’iniza hewani
9. Amwoe binti yake Aksa
10. “Alfa na Omega, mwanzo na mwisho”
11. Nguo ya gunia
12. Kimhamu
13. Kwamba alikuwa Mroma
14. Endori
15. Tete
16. Rahabu
17. Jiwe gumu
18. Kutokana na “mambo yale yaliyoandikwa katika hizo hatikunjo kulingana na vitendo vyao”
19. Shetani
20. Mashahidi wawili au watatu
21. Iriya
22. Ai
23. Kula
24. Eri na Onani
25. Sabato