Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Bora Zaidi Kuliko Kuingilia Kati kwa Mwanadamu
  • Kazi, Mkazo, na Mishiko ya Moyo
  • ‘Usafiri wa Ulimwengu wa Kufaa Zaidi’
  • Wachokozi Wazidi
  • Kuzaa kwa Njia ya Kupasuliwa au Kuzaa kwa Njia ya Kawaida?
  • Ujitoaji wa Kidini Katika Ugiriki Wapungua
  • Lisha Nyanya Barua Zako Usizozihitaji
  • Msaada kwa Wenye Maradhi ya Ngozi
  • Mazungumzo ya Wazazi kwa Watoto Wachanga—Zaidi ya Sauti za Kutuliza Tu?
  • Dhuluma Baadhi ya Visababishi na Matokeo
    Amkeni!—2003
  • Dhuluma Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003
  • Kuacha Udhalimu
    Amkeni!—2003
  • Kudhulumu—Kuna Ubaya Gani?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Bora Zaidi Kuliko Kuingilia Kati kwa Mwanadamu

Miaka kumi baada ya dhoruba kuangusha miti milioni 15 katika Uingereza katika mwaka wa 1987, ilionekana kwamba maeneo ya mwitu ambayo hayakusumbuliwa na kuingilia kati kwa mwanadamu ukuzi mpya ulikuwa wenye kuzaa sana, laripoti The Daily Telegraph. Mahali ambapo miti ilikuwa imeangushwa, mwangaza mwingi zaidi ulifikia ardhi. Hili lilifanya miti midogo na vichaka kukua kufikia urefu wa futi 20, na wadudu, ndege, na mimea pia zimeenea upesi. Miti mingi iliyoangushwa ya mwaloni na miti iitwayo yew haikuoza kama ilivyotarajiwa, na mbao zake zikiwa zimetiwa dawa, thamani yake imepanda mara tatu. Mhifadhi wa misitu Peter Raine asema: “Madhara zaidi yamefanywa [na wanadamu] wakiwa na nia nzuri ya kusafisha kuliko yaliyofanywa na dhoruba yenyewe. Mingi ya miti iliyopandwa katika vuli hiyo ilipandwa kwa haraka, vibaya, nayo ikafa.”

Kazi, Mkazo, na Mishiko ya Moyo

Mkazo wa kiakili kazini ni hatari kubwa ya pili inayoleta matatizo ya moyo na ya mfumo wa mzunguko wa damu, uvutaji-sigareti ukiwa wa kwanza, laripoti Frankfurter Rundschau. Akitolea muhtasari uchunguzi uliotolewa na taasisi ya Federal Institute for Occupational Safety and Health, katika Berlin, Ujerumani, ripoti hiyo yasema: “Wafanyakazi walio hatarini zaidi ni wale ambao hawana uhuru mwingi wa kufanya maamuzi na ambao kazi zao hazina unamna-namna. Ikiwa wanakuwa chini ya mkazo wakati wa saa za mapumziko, kwa mfano ikiwa wanajenga nyumba yao wenyewe au wanamtunza mtu wa jamaa aliye mgonjwa, hapo tisho la kupatwa na mshiko wa moyo huongezeka kufikia mara tisa.” Mtaalamu mmoja asihi sana kwamba wafanyakazi wakubaliwe kuwa na nafasi zaidi katika kufanya maamuzi. “Majadiliano mara moja tu kwa mwezi kati ya wafanyakazi wote katika idara yaweza kuboresha hali.”

‘Usafiri wa Ulimwengu wa Kufaa Zaidi’

Unaposafiri umbali wa kilometa zipunguazo nane katika sehemu ya mjini, baiskeli yaweza kuwa ya haraka zaidi kuliko gari, laripoti gazeti la habari la The Island, la Colombo, Sri Lanka. Kikundi cha mazingira cha kimataifa Marafiki wa Dunia chaita baiskeli kuwa “namna inayofaa zaidi ya usafiri Duniani.” Wanasema kwamba baiskeli yaweza kwenda mwendo wa kilometa 2,400 zisizo na uchafuzi kwa kutegemea nguvu zitokanazo na chakula zinazolingana na galoni moja ya petroli, ripoti hiyo yataarifu. Yaongezea kuwa kutumia baiskeli pia huandaa manufaa za kiafya.

Wachokozi Wazidi

Ukaguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha La Sapienza katika Roma waonyesha kwamba wanafunzi wengi hukabili namna mbalimbali za uchokozi ambazo hutia ndani matusi, kutendwa vibaya, wizi wa vitu vidogo-vidogo, uchokozi wa kimwili, na vitisho. Makosa yaliyozidi sana yalionekana hasa katika Roma, ambapo zaidi ya asilimia 50 ya wavulana na wasichana walikuwa wameteseka kutokana na visa vya kuchokozwa katika kipindi cha miezi mitatu. “Katika mazungumzo ya kindani,” aeleza mtafiti Anna Costanza Baldry, “wasichana wengi walikabili hali za kusumbuliwa kingono ambazo hawakuwa wameripoti, kwa sababu ya hofu na . . . kwa sababu wanaona tabia fulani zisizo za adili kuwa za kawaida,” likasema gazeti la habari la Italia La Repubblica.

Si watoto tu wanaochokozwa. Gazeti The Irish Times laripoti kuwa watu wazima wengi hupata kuchokozwa wakiwa kazini hasa na wakubwa wao. “Uchokozi wa maneno, uchambuzi wa kazi ya watu na kuenezwa kwa uvumi kuwahusu ni hila zipendwazo za uchokozi wa kazini,” gazeti hilo likasema. “Kutweza na kuweka miradi isiyofaa ilikuwa kawaida pia.” Kuchokoza kwahusishwa na madhara ya kisaikolojia ambayo hutia ndani “hangaiko, kutotulia, kushuka moyo, kurukwa na akili, mkazo, kupoteza uhakika, kupoteza kujistahi, na kujitenga,” lasema gazeti Times. Katika visa vilivyozidi kiasi kuchokozwa kama huku kwaweza kuongoza kwenye “kuchanganyikiwa au hata kujiua.”

Kuzaa kwa Njia ya Kupasuliwa au Kuzaa kwa Njia ya Kawaida?

Madaktari na akina mama wa Brazili mara nyingi hupendelea kuzaa kwa njia ya kupasuliwa kuliko kuzaa kwa njia ya kawaida. Daktari huona kwamba “anaweza kuzalisha akina mama wengi zaidi na anaweza kupata pesa nyingi zaidi katika ofisi yake, na hahitajiki kupoteza mwisho-juma wake,” laripoti gazeti Veja. Akina mama “huchagua kutozaa kwa njia ya kawaida, ili kuepuka uchungu (hata hivyo, kuna uchungu mwingi zaidi unaohusika kutokana na kuzaa kwa njia ya kupasuliwa), na wanaamini kuwa utaratibu huo utakuwa wenye faida kwao kimwili watakapokuwa katika udhibiti wa dawa (ambalo si kweli).” Katika hospitali za umma, thuluthi moja ya akina mama wote wanaozaa huzaa kwa njia ya kupasuliwa, na katika hospitali fulani za kibinafsi, kadirio liko juu kufikia asilimia 80. “Kuzaa kumekuwa bidhaa ya biashara,” asema Dakt. João Luiz Carvalho Pinto e Silva, msimamizi wa ukunga katika Chuo Kikuu cha Campinas. “Kwa kawaida watu husahau kwamba tofauti na kuzaa kwa njia ya kawaida, kuzaa kwa kupasuliwa ni upasuaji. Kunapoteza damu nyingi, muda wa kuwa chini ya udhibiti wa dawa ni mwingi, na uwezekano wa ambukizo waongezeka.” Kulingana na daktari, “kuzaa kwa njia ya kupasuliwa kwapasa kufanywa katika visa vitatu tu: wakati maisha ya mgonjwa au ya mtoto yako hatarini, wakati hakuna dalili za uchungu, au wakati kuna matatizo ya ghafula,” lasema Veja.

Ujitoaji wa Kidini Katika Ugiriki Wapungua

Gazeti la habari la Athens Ta Nea hivi karibuni lilichapisha rekodi ya habari waliyopata kuhusu dini katika Ugiriki iliyofanana na nyingine waliyochapisha katika mwaka wa 1963. Matokeo yaonyesha upungufu katika ujitoaji wa kidini katika nchi hiyo. Kizazi kimoja kilichopita, asilimia 66 walisema kwamba wao huenda kanisani angalau mara mbili au tatu kwa mwezi, ikilinganishwa na angalau asilimia 30 katika rekodi ya karibuni. Zaidi ya thuluthi mbili ya watu wazima 965 waliohojiwa katika eneo la jiji kuu la Athens na maeneo yanayolizunguka walisema kwamba kanisa lilitumikia umma “kidogo” au “halikutumikia kabisa,” waandishi wa habari wa Reuters waripoti. Akiandika katika Ta Nea, mwandishi mashuhuri Mgiriki Elias Nikolakopoulos alisema kuhusu “kuondoa umma wa Ugiriki polepole kutoka kwenye dini,” akisema kwamba sasa kuna “hadhari na uchungu wa moyo” kuelekea kanisa katika Ugiriki.

Lisha Nyanya Barua Zako Usizozihitaji

Ofisi ya posta yaweza kufanya nini na tani 500 za barua zisizohitajika ambazo haziwezi kupelekwa kwa watu, zikitia ndani katalogi na matangazo mengine? Ofisi ya posta ya Dallas-Fort Worth, Texas, imeanza kutuma nyingi zazo zikafanywe kuwa mbolea ya mchanganyiko. Mbolea hiyo ya mchanganyiko inatumiwa kukuzia nyanya na mimea aina ya marigold, laripoti The New York Times, na matokeo yamekuwa yenye kupendeza. Bakteria ambazo hubadilisha barua zisizohitajika ambazo zimechanwa kuwa mbolea ya mchanganyiko hunyweshwa pombe iliyochacha na vinywaji vitamu, takataka za watengenezaji wa vinywaji. Pombe na soda huwa na sukari, ambayo huchangia kusitawi kwa bakteria. Joel Simpson, makamu wa msimamizi wa kampuni inayoendesha jaribio hilo asema: “Vitu vilevile vinavyotufanya tunenepe hufanya bakteria kunenepa na kufurahi.”

Msaada kwa Wenye Maradhi ya Ngozi

“Watu wengi wanaoteseka kutokana na matatizo ya ngozi hawatafuti matibabu kwa sababu ya kuaibika na wanaweza kuishi kwa miaka mingi ‘wakiteseka kimya,’” laripoti gazeti The Irish Times. Akikazia hali yao mbaya Dakt. Gillian Murphy asema: “Ninao wagonjwa ambao wanaugua kutokana na psoriasis, ambao ngozi yao kihalisi huanguka wanapovua nguo, na wanajihisi kuwa wasio safi na kuaibika hivi kwamba hawawezi kukaa katika hoteli au kwenda kwa mtengeneza-nywele.” Bill Cunliffe, profesa mtaalamu wa ngozi katika Chuo Kikuu cha Leeds aongezea: “Chunusi huwaathiri watu kimwili na kiakili. Kwa kawaida hiyo hufikiriwa kuwa chafu na yenye kuambukiza. Ikiwa watu wawili wenye uwezo sawa wameenda kwa mahojiano ya kutafuta kazi, yule ambaye hana chunusi atapata kazi.” Cunliffe asema kwamba amekuwa na wagonjwa fulani ambao wamekuwa na vurugu la akili kwa sababu ya kuwa na chunusi ambao wamejaribu kujiua. Madaktari katika Mkutano wa Shule ya Elimu ya Ngozi na Magonjwa Yanayoambukizwa Kingono ya Ulaya katika Dublin, Ireland, walisisitiza umuhimu wa kutafuta matibabu mapema. “Ni tatizo kubwa kwa watu fulani,” akasema daktari mmoja, “lakini ni muhimu kukumbuka kwamba kuna matibabu mazuri sana yawezayo kupatikana.”

Mazungumzo ya Wazazi kwa Watoto Wachanga—Zaidi ya Sauti za Kutuliza Tu?

Wanasayansi fulani wasema kuwa wazazi wanaowanong’onezea watoto wao waweza kuwa wanawapa zaidi ya shauku nyororo tu. Patricia Kuhl, wa Chuo Kikuu cha Washington, pamoja na wafanyakazi wenzake walichunguza misemo iliyoelekezwa kwa watoto ya lugha tatu mbalimbali—Kirusi, Kisweden, na Kiingereza. Inaelekea kwamba namna ya msemo wa wazazi uliotiliwa chumvi hauvutii tu uangalifu wa mtoto bali pia hutumika kama msingi kwa mtoto kujifunza lugha hiyo. “Kufikia umri wa miezi 6,” lasema gazeti Science, “watoto wachanga hujifunza kuainisha sauti za vokali, wakikazia uangalifu tofauti ambazo ni za maana katika lugha yao ya asili, kama vile tofauti kati ya ‘ee’ na ‘ah’ huku wakipuuza tofauti zisizo za maana.” Süddeutsche Zeitung, uchunguzi huo ulifikia mkataa kwamba utumizi wa simu za kushikwa mkononi unapoendesha gari “hutokeza hatari kubwa kwa usalama.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki