Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa,na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Kwa sababu ya daraka la Yesu la kidhabihu, Yohana Mbatizaji alimtambulisha Yesu kuwa nani? (Yohana 1:29)
2. Ni nchi ipi iliyo “pande za mwisho za kaskazini” ambako jeshi la Gogu hutoka? (Ezekieli 38:2, 15)
3. “Mashirika mabaya” huharibu nini? (1 Wakorintho 15:33)
4. Ni katika njia gani ‘nguvu za watu wakomavu huzoezwa kutofautisha lililo sahihi na lililo kosa pia’? (Waebrania 5:14)
5. Walipokuwa wakijaribu kunyakua umaliki, Absalomu na Adonia walifanya nini? (2 Samweli 15:1; 1 Wafalme 1:5)
6. Kulingana na Paulo, ni nini hakingeweza kuuambia mkono: “Sikuhitaji wewe”? (1 Wakorintho 12:21)
7. Baba ya Yoshua alikuwa nani? (Yoshua 1:1)
8. Mika alitabiri kwamba katika siku za mwisho, ‘mlima wa nyumba ya BWANA ungewekwa imara’ juu ya nini? (Mika 4:1)
9. Ni mahali gani Akani na nyumba yake walipopigwa kwa mawe hadi wakafa? (Yoshua 7:24)
10. Akikazia uhitaji wa imani, ni nini ambacho Paulo alisema lazima mtu aamini kuhusu Mungu? (Waebrania 11:6)
11. Mjukuu wa Kaini alikuwa nani? (Mwanzo 4:18)
12. Ukoo wa Mfalme Sauli ulikuwa upi? (1 Samweli 9:21)
13. Ni kupitia nabii yupi Mungu alimwambia Daudi achague moja kati ya adhabu aina tatu kwa sababu ya kufanya kimbelembele kuwahesabu watu? (1 Mambo ya Nyakati 21:9-12)
14. Ni nani walio na hatia ya kufanya uasherati na Babiloni Mkubwa? (Ufunuo 17:2)
15. Ni mwezi upi alioagiza Yehova kuwa wa kwanza katika kalenda takatifu ya Kiyahudi? (Esta 3:7)
16. Ni nani aliyeongoza muungano wa wafalme walioteka mpwa wa Abrahamu, Loti? (Mwanzo 14:9)
17. Ni mavazi gani mawili yaliyotajwa ambayo yalimfanya Ahazia atambue kwamba ni Eliya aliyetuma ujumbe kwamba angefia kitanda hicho alichokilalia? (2 Wafalme 1:8)
18. Ndugu za mwanamwali Mshulami walimpa kazi gani, iliyofanya ngozi yake iunguzwe? (Wimbo Ulio Bora 1:6)
19. Ni mwendelezo upi wa jina la Mungu unaopendelewa na wasomi wengi?
20. Ni jina lipi alilopewa Mwanavita-Mfalme, Yesu, lililoandikwa kwenye vazi lake la nje? (Ufunuo 19:16)
Majibu ya Maswali
1. “Mwana-kondoo wa Mungu ambaye huondolea mbali dhambi ya ulimwengu”
2. Magogu
3. “Mazoea yenye mafaa”
4. “Kupitia utumizi”
5. Kila mmoja alijiwekea mwenyewe gari na farasi na watu 50 wa kupiga mbio mbele yake
6. Jicho
7. Nuni
8. “Juu ya milima”
9. Katika bonde la Akori
10. “Kwamba yeye yuko na kwamba yeye huwa mthawabishaji wa wale wanaomtafuta kwa bidii”
11. Iradi
12. Kabila ya Benyamini
13. Gadi
14. “Wafalme wa dunia”
15. Nisani
16. Kedorlaoma, mfalme wa Elamu
17. Vazi la manyoya na shuka ya ngozi
18. Mlinzi wa mashamba ya mizabibu
19. Yahweh
20. “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana”