Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 11/8 uku. 32
  • “Amkeni! Lina Habari Bora”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Amkeni! Lina Habari Bora”
  • Amkeni!—1998
Amkeni!—1998
g98 11/8 uku. 32

“Amkeni! Lina Habari Bora”

Hayo yalikuwa maelezo ya mvulana Mwislamu mwenye umri wa miaka 16 kutoka Benin City, katika nchi ya Afrika ya Nigeria. Alitoa maelezo haya kupitia barua aliyoandikia ofisi ya tawi ya Nigeria ya Mashahidi wa Yehova:

“Nilipata magazeti ya Amkeni! katika nyumba ya rafiki mmoja nikaomba matoleo tisa. Niliyasoma yote kutoka jalada hadi jalada kwa siku moja! Naandika kusifu akili zote zilizotumika kuandika Amkeni!—kutia ndani Yehova—kwa kazi hii nzuri sana! Navutiwa hasa na jinsi mnavyounganisha masuala ya kimazingira pamoja na Biblia na Mungu. Nikiwa mshiriki wa Shirika la Uhifadhi la Nigeria, nimekuwa nikitafuta habari ili kujaza maktaba yangu ya mazingira na ya mali-asili. Sasa natambua kwamba Amkeni! lina habari bora. Tafadhali nijulisheni jinsi ninavyoweza kupata matoleo mawili ya Amkeni! kila mwezi moja kwa moja kutoka kwenu.”

Labda hujapata kusoma Amkeni! kabla ya kuona hili. Ikiwa ungependa kupokea nakala nyingine, tafadhali toa ombi hilo kwa kuandikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au kwa kutumia anwani ihusuyo katika ukurasa wa 5. Tutafurahi kukupelekea nakala nyingine, au ukiomba, mtu fulani aweza kukutembelea nyumbani kwako kuchunguza pamoja nawe umaana wa nyakati tunamoishi.

□ Nipelekeeni nakala ya karibuni ya Amkeni!

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Tufe: Courtesy of Replogle Globes, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki