Ukurasa wa Pili
Ushirikina—Kwa Nini Ni Hatari Sana? 3-11
Mbali na kwamba tunaishi katika enzi yenye shuku, yaonekana kwamba ushirikina umeenea kuliko wakati mwingineo wote. Kwa nini? Je, zoea linaloonekana kuwa la kawaida na linalopendwa na wengi kwa kweli laweza kuwa hatari?
Kuishi na Maradhi ya Cystic Fibrosis 12
Jifunze juu ya ugonjwa huu wa kurithiwa usiokuwa na tiba na jinsi ambavyo mwanamume mmoja kijana anakabiliana nao.
Mto Danube—Laiti Ungeweza Kuzungumza! 15
Mto Danube una habari ya kusimulia—ya tamaduni mbalimbali, visa mbalimbali vya kihistoria ambavyo kwa kawaida ni vya umwagaji wa damu, na tisho la uchafuzi wa siku ya kisasa.