Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g00 8/22 uku. 31
  • Msaada wa Kuacha Uhalifu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msaada wa Kuacha Uhalifu
  • Amkeni!—2000
  • Habari Zinazolingana
  • Kuna Tumaini Gani kwa Majiji?
    Amkeni!—2001
  • Kuharibu Vitu Kimakusudi Kunaweza Kukomeshwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Kwa Nini Watu Wengi Sana Huishi kwa Woga?
    Amkeni!—2005
  • Sababu Inayowafanya Wawe Wajeuri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2000
g00 8/22 uku. 31

Msaada wa Kuacha Uhalifu

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UFARANSA

MATUKIO ya hivi karibuni yameonyesha sana uvunjaji wa sheria na ukosefu wa kufuata utaratibu katika maeneo mengi yenye umaskini katika miji ya Ufaransa. Kulingana na gazeti la Ufaransa L’Express, “jeuri katika miji imeongezeka mara tano kwa miaka sita.” Isitoshe, idadi ya watoto wanaohusika katika uhalifu wenye jeuri imeongezeka sana.

Zaidi ya kushiriki katika kuharibu vitu kimakusudi, ulanguzi wa madawa ya kulevya, unyang’anyi, uchomaji wa mali kimakusudi, na wizi, wahalifu wamekuwa wakiwalenga hasa wafanyakazi wa umma. Polisi, zimamoto, na watumishi wa usafiri wa umma, miongoni mwa wengine hufanyiwa jeuri kwa ukawaida.

Kwa nini kuna jeuri nyingi hivyo? “Muungano wa familia ukiwa umeporomoka, huu ni uasi dhidi ya mambo yote yanayohusika na mamlaka,” waeleza wanasoshiolojia wawili. Pia wanataja kwamba “vijana wanahisi kwamba mamlaka haziwajali” na kuwa hawana “tazamio la wakati ujao wenye maana.”

Mashahidi wa Yehova wanahubiri kwa ukawaida ujumbe wa Biblia wenye tumaini katika maeneo yenye uhalifu mwingi. Katika kipindi kimoja cha televisheni huko Ufaransa hivi karibuni, mwandishi mmoja wa habari alisema hivi: “Mashahidi wa Yehova huzuru tena na tena vitongoji na maeneo ya umaskini—maeneo ambayo nyakati nyingine huonekana kana kwamba yamepuuzwa na huduma za jamii, polisi, na serikali. Katika nyumba hizo na barabara hizo, wao huongea na kusikiliza.” Kazi yao husaidia sana, kama inavyoonyeshwa na barua inayofuata kutoka kwa msomaji mmoja mchanga wa Amkeni!

“Ninawashukuru kwa moyo wangu wote kwa sababu ya vichapo vyenu. Mmenisaidia mimi binafsi na vilevile uhusiano wangu na wazazi umeboreka. Mimi ni Mwislamu na nina umri wa miaka 16.

“Ninalotaka kusema ni kuwa mmefaulu kunitoa katika maisha ya uhalifu. Tokeo ni kwamba najitoa zaidi kwa dini yangu, lakini pia nasoma Biblia. Kwa sababu yenu ninaendelea kwenda shule. Isitoshe, watu kadhaa katika eneo letu wamesaidiwa kuacha uhalifu kupitia magazeti yenu, ambayo nawaazima kila mwezi. Nawashukuru sana na ninahisi nikiwa mwenye deni.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki