Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 11
  • Upinde wa Mvua wa Kwanza

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Upinde wa Mvua wa Kwanza
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Je, Mungu Atauharibu Ulimwengu Tena Kwa Maji?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Simulizi la Noa na Gharika Kuu—Je, Ni Hekaya Tu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Onyo la Wakati Uliopita
    Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 11
Upinde wa mvua wa kwanza,  Safina ya Nuhu imetua kwenye nchi kavu

HADITHI YA 11

Upinde wa Mvua wa Kwanza

UNAJUA jambo la kwanza ambalo Nuhu alifanya wakati yeye na jamaa yake walipotoka katika safina? Alimtolea Mungu zawadi. Unaweza kumwona akifanya hivyo katika picha iliyo chini. Nuhu alitoa zawadi hiyo ya wanyama ili amshukuru Mungu kwa kuokoa jamaa yake katika gharika kuu.

Unadhani Yehova alipendezwa na zawadi hiyo? Ndiyo. Alimwahidi Nuhu kwamba hangeuharibu ulimwengu tena kwa gharika.

Nuhu na familia yake wanatoa dhabihu ili kumshukuru Yehova

Upesi nchi yote ikakauka, Nuhu na jamaa yake wakaanza kuishi tena nje ya safina. Mungu akawabarikia na kuwaambia: Zaeni watoto wengi. Mwongezeke mpaka watu waishi pote duniani.’

Lakini baadaye, labda watu wangeogopa kwamba gharika kama hiyo ingetokea tena. Basi Mungu alitoa kitu cha kukumbusha watu ahadi yake kwamba hataifunika tena dunia yote kwa maji. Unajua ni kitu gani? Upinde wa mvua.

Umepata kuuona? Unaona mmoja katika picha hii?

Mungu aliahidi hivi: Watu wote na wanyama hawataharibiwa tena kwa gharika. Ninaweka upinde wangu wa mvua katika wingu. Upinde wa mvua utakapoonekana, nitauona nikumbuke ahadi yangu.’

Basi unapoona upinde wa mvua, unakukumbusha nini? Ahadi ya Mungu kwamba hatauharibu ulimwengu tena kwa gharika kuu.

Mwanzo 8:18-22; 9:9-17.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki