Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 6 uku. 20-uku. 21 fu. 5
  • Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Maji Yachukua Ulimwengu
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Safina ya Noa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Gharika Kuu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Nuhu Anajenga Safina
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 6 uku. 20-uku. 21 fu. 5
Safina inaelea juu ya maji mvua inaponyesha

SOMO LA 6

Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya

Noa, familia yake, na wanyama wakitoka katika safina

Noa, familia yake, na wanyama waliingia ndani ya safina. Kisha, Yehova aliufunga mlango na mvua ikaanza kunyesha. Mvua hiyo ilikuwa nyingi sana hivi kwamba safina ilianza kuelea. Hatimaye, dunia yote ikajaa maji. Watu wote wabaya waliokuwa nje ya safina walikufa. Lakini Noa na familia yake walikuwa salama ndani ya safina. Je, unaweza kuwazia jinsi walivyokuwa na furaha kwa sababu walimtii Yehova?

Mvua ilinyesha kwa siku 40 mchana na usiku, kisha ikaacha. Hatua kwa hatua maji yakaanza kupungua. Mwishowe, safina ikatua juu ya milima. Hata hivyo, kulikuwa na maji mengi katika maeneo yote, kwa hiyo Noa na familia yake hawakuweza kutoka nje ya safina.

Hatua kwa hatua, maji yalikauka. Noa na familia yake walikaa ndani ya safina kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kisha, Yehova aliwaambia watoke ndani ya safina na kuingia katika ulimwengu ulionekana kuwa mpya. Walimshukuru sana Yehova kwa kuwaokoa na walifanya hivyo kwa kumtolea dhabihu.

Upinde wa mvua

Yehova alifurahishwa na dhabihu yao. Naye aliahidi kwamba hataharibu tena vitu vyote katika dunia kwa gharika. Ili kuthibitisha ahadi yake, alifanya upinde wa mvua uonekane angani kwa mara ya kwanza. Je, umewahi kuuona upinde wa mvua?

Baadaye, Yehova alimwambia Noa na familia yake wazae watoto na kuijaza dunia.

“Noa aliingia ndani ya safina; nao [watu] hawakujali mpaka Gharika ikaja na kuwafagilia mbali wote.”​—Mathayo 24:38, 39

Maswali: Ni nini kilichotokea baada ya Yehova kufunga mlango wa safina? Upinde wa mvua unatukumbusha nini?

Mwanzo 7:1–9:17

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki