Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 8
  • Kumkimbia Mtawala Mkatili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kumkimbia Mtawala Mkatili
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Makimbio ya Kuepa Mtawala wa Kutumia Mabavu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Wanaokoka kutoka kwa Mtawala Mwovu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yehova Alimlinda Yesu
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Aliilinda Familia Yake, Akawaandalia, na Akavumilia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 8

Sura 8

Kumkimbia Mtawala Mkatili

YUSUFU amwamsha Mariamu kumpa habari zenye uharaka. Malaika wa Yehova amemtokea sasa hivi tu, akimwambia: “Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.”

Upesi, hao watatu wakimbia. Nao wafanya hivyo kwa wakati ufaao kwa sababu Herode amejua kwamba wale wanajimu wamemfanyia ujanja na kuondoka nchini. Kumbuka, walipaswa kurudi kwake wakiisha kumpata Yesu. Herode aghadhibika. Hivyo katika jaribio la kumuua Yesu, atoa amri wauawe wavulana wote wenye umri wa miaka miwili kurudi chini katika Bethlehemu na wilaya zake. Msingi wa kufanya hesabu yake ya umri ni ile habari aliyopata mapema kidogo kutoka kwa wale wanajimu wa kutoka Mashariki.

Machinjo ya watoto wote wavulana ni jambo linalochukiza sana kuona! Askari wa Herode wavunja na kuingia nyumba moja baada ya nyingine. Nao wakimpata mtoto mvulana, wanamnyakua mikononi mwa mama yake. Hatujui ni watoto wangapi wanaowaua, lakini kilio na majonzi makubwa ya akina mama yatimiza unabii ulio katika Biblia wa Yeremia nabii wa Mungu.

Wakati huu, Yusufu na familia yake wamekwisha kufika Misri wakiwa salama, nao wanaishi huko sasa. Lakini usiku mmoja kwa mara nyingine malaika wa Yehova amtokea Yusufu katika ndoto. “Ondoka, umchukue mtoto na mamaye,” asema malaika huyo, “ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho [nafsi, NW] ya mtoto.” Kwa hiyo, kwa utimizo wa unabii mwingine wa Biblia unaosema kwamba Mwana wa Mungu angeitwa atoke Misri, familia hiyo yarudi kwenye nchi ya kwao.

Yaonekana Yusufu akusudia kufanya makao katika Yudea, walikokuwa wakiishi katika mji wa Bethlehemu kabla ya kutorokea Misri. Lakini apata habari kwamba Arkelao, mwana mwovu wa Herode, sasa ni mfalme wa Yudea, na katika ndoto nyingine Yehova amwonya juu ya hatari hiyo. Kwa hiyo Yusufu na familia yake wasafiri kaskazini na kufanya makao katika mji wa Nazareti katika Galilaya. Yesu akulia katika mtaa huo, mbali na makao makuu ya maisha ya kidini ya Wayahudi. Mathayo 2:13-23; Yeremia 31:15; Hosea 11:1.

▪ Wanajimu wakosapo kurudi, Mfalme Herode afanya jambo gani baya sana, lakini Yesu alindwaje?

▪ Warudipo kutoka Misri, ni kwa nini Yusufu hakai tena katika Bethlehemu?

▪ Ni unabii gani mbalimbali wa Biblia watimizwa wakati wa kipindi hicho?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki