Wimbo Na. 146
Mlinitendea Mimi
Kondoo wengine, wanatumikia
bega kwa bega na ndugu za Kristo.
Wanapowasaidia
ndugu zake
Yesu anasema atawalipa.
(KORASI)
“Mlipowatunza, mlinitunza.
Kwa kuwafariji, mwanifariji.
Bidii yenu kwa ajili yao.
Mnapotenda mema yoyote.
Mnanitendea mema na mimi.”
“Wakati wa njaa, wakati wa kiu
nilichohitaji, mliandaa.”
“Bwana tulikufanyia
hayo lini?”
Na ndipo Mfalme atawajibu:
(KORASI)
“Mlipowatunza, mlinitunza.
Kwa kuwafariji, mwanifariji.
Bidii yenu kwa ajili yao.
Mnapotenda mema yoyote.
Mnanitendea mema na mimi.”
“Ushikamanifu mmenionyesha,
kwa kuhubiri na kwa kazi njema.”
Kisha Yesu atabariki
kondoo:
“Rithini dunia pia uzima.”
(KORASI)
“Mlipowatunza, mlinitunza.
Kwa kuwafariji, mwanifariji.
Bidii yenu kwa ajili yao.
Mnapotenda mema yoyote.
Mnanitendea mema na mimi.”
(Ona pia Met. 19:17; Mt. 10:40-42; 2 Tim. 1:16, 17.)