WIMBO NA. 161
Ninafurahia Kufanya Mapenzi Yako
1. Mwanao alipobatizwa
Ulimpa Neno lako,
Lilimchochea moyoni
Atimize kusudi.
Aliyapinga majaribu.
Kakweza jina lako.
Alijitoa kikamili,
Natamani kumwiga.
(KORASI)
Mapenzi yako n’tafanya.
Nakupa nguvu na moyo.
Ninapata shangwe nyingi.
Kutembea nuruni.
Mapenzi yako n’tafanya.
Tumaini ni hakika.
Wanipenda Ee Yehova.
Nitakusifu wewe.
Nitafanya.
2. Nilipokujua Yehova,
Niliridhika moyoni.
Nitakutetea kwa shangwe,
Kweli yako sifichi.
Kutumika na ndugu zangu,
Maisha bora sana.
Sihofu kuitwa Shahidi.
Nakupa nafsi yangu.
(KORASI)
Mapenzi yako n’tafanya.
Nakupa nguvu na moyo.
Ninapata shangwe nyingi.
Kutembea nuruni.
Mapenzi yako n’tafanya.
Tumaini ni hakika.
Wanipenda Ee Yehova.
Nitakusifu wewe.
Nitafanya.
Yote nitafanya.