Waokolewa Wasichinjwe Pamoja na Adui za Mfalme
1. Kumkataa kwetu Mfalme mpya wa dunia sasa kwaweza kumaanisha matokeo gani, kulingana na mfano gani wa kuonya wa kale?
TUKIWA tunaishi katika “wakati wa mwisho” wa “taratibu ya mambo” iliyopo, yaweza kumaanisha matokeo mabaya sana sana kwetu tukimkataa Mfalme mpya wa dunia. (Dan. 12:4; Mt. 24:3, NW) Miaka 1,900 iliyopita matokeo yalikuwa mabaya sana kwa Waisraeli waliokuwa wakiishi katika mwisho wa taratibu ya mambo ya Kiyahudi iliyouzunguka Yerusalemu na hekalu lake. (Ebr. 9:26) Huo ulikuwa mfano wa kutuonya sisi leo. Onyo hili linakaziwa kwa ajili yetu katika mfano wa Yesu wa kabaila aliyewakabidhi kumi wa watumwa wake mina kumi za fedha.
2. Yesu aliondoka wakati gani kama aliyetazamiwa kuwa Mfalme, na “raia” wenzake waliopaswa kupeleka wajumbe wamfuate wakaupinge ufalme wake walikuwa akina nani?
2 Katika mfano Yesu anaendelea kusema: “Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.” (Luka 19:14) Ni alipokwisha kufufuliwa kutoka kwa wafu kwamba Yesu kama yeye aliyetiwa mafuta na roho takatifu ya Mungu awe Mfalme wa Kimasihi akapaa kutoka duniani kwenda mbinguni, siku kumi tu mbele ya sikukuu ya Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E. Kulingana na taifa la kimwili la Yesu, “watu wa mji wake” walikuwa ndio Waisraeli au Wayahudi. Kulingana na uhakika huu imeandikwa: “Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana.” (Gal. 4:4, 5) “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” (Yohana 1:11) Basi, sasa, Yesu alipokwisha kupaa mbinguni, raia wenzake wa Kiyahudi walitumaje wajumbe kumfuata ili wakakatae Yesu asitumie uwezo wa kifalme juu yao?
3. Kwa kuwa “raia” wenzake walikuwa wenye nyama na damu, wangewezaje kupeleka wajumbe “kumfuata” wakaukatae ufalme wake?
3 Wakiwa wenye nyama na damu, hakuna kundi la wajumbe wa Kiyahudi ambao wangeweza kwenda mbinguni na kuonekana mbele za Mungu mahali palipo patakatifu na kumwambia asimpe Mwanawe Yesu aliyefufuliwa ufalme wa Kimasihi. Lakini haikuwa lazima wafanye hivyo. Walimtangazia Mungu kwa matokeo yale yale. Namna gani? Ilikuwa ni tangu sikukuu ya Pentekoste na kuendelea, kwa maana wakati huo wanafunzi wa Kikristo waliokuwa wakienda “chinichini” walitokea nje. Ndio wakati huo mtume Petro, akitenda kama mnenaji kwa ajili ya karibu wanafunzi 120, alipohutubia Wayahudi zaidi ya elfu tatu waliokusanyika katika Yerusalemu: “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.” (Matendo 2:36) Lakini je! wenye mamlaka wa kidini katika Yerusalemu walikubaliana na tangazo hilo la Yesu kama Masihi? Sivyo, iwapo upinzani wao na mateso juu ya wanafunzi wake Yesu kufuata hapo vinaonyesha hivyo. Kwa hiyo kwa kukataa kwao rasmi ushuhuda uliotolewa na wanafunzi kwamba Yesu hakuwa ndiye Masihi wa Mungu aliyeahidiwa, walikuwa wakimtangazia Mungu mbinguni kwamba wao hawakumtaka Mwana wake aliyefufuliwa kama Mfalme wao wa Kimasihi.—Matendo 5:34-39.
4. (a) Kwa kumkataa Yesu kama mfalme wa Kimasihi, “raia” za Kiyahudi walijiacha wafanywe nini? (b) Hii iliwaelekeza “raia” hao kwenye matokeo gani nyumaye, lakini ikatukiaje kwa Wayahudi waliogeuzwa wakawa Wakristo?
4 Raia wenzi wake Yesu walikuwa na maoni yao wenyewe juu ya n’nani amepaswa kuwa mfalme wao katika cheo cha Masihi. Hivyo walijiacha wadanganywe na Masihi wa uongo, Makristo wa uongo. Ni chini ya mawazo ya uongo ya Kimasihi kwamba Wayahudi wenye kutukuza taifa waliasi katika mwaka wa 66 C.E. juu ya Kaisari asiwe tena kama mfalme wao. (Yohana 19:15) Miaka michache ya kujitegemea walikokupata kwa Milki ya Kirumi ilimalizika wakati Yerusalemu na hekalu lake ulipoachwa kama magofu katika mwaka wa 70 C.E. Maelfu ya Wayahudi waliofanywa Wakristo walishukuru kwamba hawakuwa wamedanganywa kujiunga na maasi ya Kiyahudi ya Kimasihi, nao waliendelea ‘kufanya biashara’ na mina za fedha za mfano walizopewa na Yesu Kristo mbele ya kuondoka kwake kuelekea kwenye “nchi ya mbali” ya kimbinguni. Hawakupoteza cho chote kwa kiroho kwa njia ya uharibifu wenye kuogofya wa Yerusalemu na kwa njia ya kutawanywa kwa ukatili kwa Wayahudi wasioamini.
KUFANYA BIASHARA NA MALI YA MFALME
5. Katika mfano, wakati kabaila aliyerudi alipoanza kufanya hesabu na watumwa wake, aliyetokea kwanza alisema nini?
5 Katika mfano wa Yesu, “kabaila” anapokwisha tu kurudi kutoka safari yake ndefu ya mbali, ndipo tunapojifunza mambo waliyoyafanya watumwa wake kumi na mina za fedha walizokabidhiwa. Twasoma: “Hatimaye aliporudi baada ya kujipatia uwezo wa kifalme [au, ufalme], aliamuru wakaitwe mbele yake watumwa hawa aliokuwa amewapa fedha, kusudi ahakikishe walichokuwa wamepata kama faida kwa biashara yao. Kisha wa kwanza akajitokeza, akisema, ‘Bwana, mina yako imepata faida ya mina kumi.’ “(Luka 19:15, 16, NW) Kulingana na An American Translation mtumwa huyu alisema: “Shilingi zako mia moja na arobaini zimefanyiza shilingi elfu moja na mia nne, bwana!” Kulingana na tafsiri ya Moffatt, alisema: “Shilingi zako mia moja zimefanyiza nyingine elfu moja, bwana.” Yeye alipata faida mara kumi ya aliyokuwa amepewa.
6. (a) Mtumwa wa kwanza alifananisha nini? (b) Biashara ilifanywaje na “mina” ya fedha ya Bwana tangu Pentekoste na kuendelea?
6 Kwa kuwa ‘watumwa kumi’ wa mfano waliwafananisha wanafunzi wote wa Yesu Kristo waliotiwa mafuta na kuzaliwa kwa roho tangu Pentekoste ya mwaka wa 33 C.E. mpaka sasa, mtumwa huyu wa kwanza alifananisha jamii au kikundi cha wanafunzi hao wa Kikristo. Bila shaka, mitume kumi na wawili waaminifu na mtume Paulo walikuwa wa jamii hii. Wakiwa mitume au “waliotumwa,” bila shaka walilipanua shamba lao lililokuwa likisitawishwa alilokuwa ameliacha Bwana wao Yesu Kristo kama jambo lenye thamani na lenye mazao la kuanzia kufanya kazi au kufanya biashara. Namna ambavyo wao walivyofanya biashara na mina ya fedha ya mfano kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha. Tangu sikukuu ya Pentekoste na kuendelea twasoma juu ya “fundisho la mitume” ambalo kwalo waamini wa Kikristo walijitoa, na kwamba “ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume,” na kwamba “[Yehova] akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.”—Matendo 2:42, 43, 47.
7. Walipokuwa matesoni, mitume walifanya nini, kwa mfano walipokwisha kuwamo katika Sanhedrin (Baraza Kuu) ya Yerusalemu?
7 Mitume waliiendeleza kazi yao ya kuhubiri na kufundisha, wajapokuwa waliadhibiwa isivyo haki kwa kufanya hivyo. Kwa mfano, hili ndilo lililotukia mitume walipokwisha kuwa na kesi yao mbele ya Sanhedrin (Baraza Kuu) ya Yerusalemu: “Wakawaamuru mitume wafike barazani, wakawapiga mijeledi, na kuwaagiza waache kusema juu ya msingi wa jina la Yesu, na kuwaacha waende. Hawa [mitume], basi, wakaenda zao kutoka Baraza Kuu, wakifurahi kwa kuwa walikuwa wamehesabiwa wanastahili kudhulumiwa kwa ajili ya jina lake. Na kila siku hekaluni na nyumba kwa nyumba wakaendelea bila ya kuchoka wakizifundisha na kuzitangaza habari njema juu ya Kristo, Yesu [au, Yesu Masihi].”—Matendo 5:40-42, New World Translation; New English Bible; New American Bible; tazama vile vile Moffatt.
8. Kwa sababu ya kushikamana sana kwa mitume na kuhubiri na kufundisha, nini kilichotukia kwa habari ya hesabu ya waamini?
8 Katika kushikamana sana na huduma yao, mitume kumi na wawili waliliambia kundi la Yerusalemu: “Sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.” (Matendo 6:4) Si ajabu kwamba kufuata hapo twasoma: “Neno la Mungu likaenea [kwa kuhubiri na kufundisha]; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.” Sasa hesabu ya waamini lazima iwe ilikwisha kupanda kupita 5,000, kwa maana wakati fulani mapema zaidi twasoma: “Wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya watu waume ikawa kama elfu tano.”—Matendo 6:7; 4:4.
9, 10. (a) Shamba la kulimwa lilipanuliwaje, kulingana na Matendo, sura ya nane mpaka ya kumi? (b) Mtume Paulo anatoa maelezo gani juu ya namna alivyofanya biashara na mina ya fedha ya mfano?
9 Kufuata hapo, kutoka Yerusalemu kama msingi wa utendaji, shamba la utendaji lilienezwa kwenye Wasamaria waliotahiriwa, na kwenye mwongofu aliyetahiriwa wa Kiethiopia, kisha, katika wakati wa Mungu uliowekwa, kwenye watu wote wasio Wayahudi waliotahiriwa au Mataifa. (Matendo sura za 8-10) Penye mkutano wa baraza inayoongoza ya Kikristo katika Yerusalemu, mwanafunzi Yakobo alitoa maelezo juu ya mpanuko wa shamba la kusitawishwa ili kuutia ndani ulimwengu wa Mataifa, akisema: “Simeoni [Petro] ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili jina lake. Na maneno ya manabii yapatana na hayo.” (Matendo 15:14, 15) Wakati huu ulipopita mtume Paulo alifunga safari yake ya pili ya umisionari na kupenya katika Ulaya. Juu yake mwenyewe, Paulo alisema: “Kwa maana mimi, kwa hakika, ni mtume kwa mataifa, naitukuza huduma yangu.” (Rum. 11:13, NW) Katika safari yake ya tatu ya kurudi ya umisionari, Paulo alieleza namna ambavyo alifanya biashara na mina ya fedha ya mfano aliyokuwa amekabidhiwa na Bwana Yesu Kristo, akiwaambia hivi wazee wa kundi la Efeso, Asia Ndogo:
10 “Sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa, bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba [au, hadharani au katika nyumba zenu, AT, NE, Rotherham; hadharani au faraghani, NA], nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.”—Matendo 20:20, 21.
11. Kama matokeo ya kufanya biashara kwa watumwa wa Kikristo na mina ya mfano, ni ushuhuda wa kadiri gani uliokuwa umetolewa mbele ya uharibifu wa Yerusalemu?
11 Kwa hiyo, basi, je! huko nyuma katika karne ya kwanza mitume na wanafunzi wenzao waliotiwa mafuta waliziongeza mina za mfano walizokuwa wamekabidhiwa na Bwana Yesu Kristo kama watumwa wake wa Kikristo? Ndiyo, walifanya hivyo. Hapa tunao ushuhuda ulioandikwa wa mtume Paulo, alipoiandika barua yake kwa Wakolosai akiwa katika nyumba yake ya kifungo katika Rumi karibu miaka kumi mbele ya uharibifu wa Yerusalemu katika mwaka wa 70 C.E., akizungumza juu ya maenezi ya habari njema: “Habari njema hizo zilizojitokeza kwenu, hata kama vile zinavyozaa matunda na kuongezeka katika ulimwengu wote . . . habari njema hizo mlizozisikua, na zilizohubiriwa katika kuumba kote kuliko chini ya mbingu.” (Kol. 1:5, 6, 23, NW) Hivyo, miaka mingi mbele ya mwisho wa taratibu ya mambo ya Kiyahudi iliyouzunguka Yerusalemu, ushuhuda wa ulimwengu ulikuwa umekwisha kutimilizwa.
KUFANYA BIASHARA NA “MINA” KATIKA KARNE YA 20
12. (a) Kwa sababu gani Kristendomu hastahili kuhesabiwa sifa kwa ajili ya “kuongezeka katika ulimwengu wote” kwa “habari njema hizo”? (b) Nani anayestahili kupewa sifa, na kwa sababu gani?
12 Leo, ikiisha kupita miaka 1,900, je! vile vile yaweza kusemwa kwamba habari njema ‘zinaongezeka katika ulimwengu wote’ na kwamba zimekwisha kuhubiriwa katika kuumba kote kuliko chini ya mbingu’? Ndiyo, zaidi hivyo kuliko katika karne ya kwanza C.E. Sifa kwa ajili ya hili haipaswi kupewa kwa Kristendomu mwenye umri wa zaidi ya karne kumi na sita sasa. Yeye na mamia ya mamilioni ya washiriki wake wa makanisa hawatangazi kwamba Bwana Yesu Kristo alijipatia ‘uwezo wake wa kifalme’ mwishoni mwa Majira ya Mataifa katika mwaka wa 1914, mwaka wa Vita ya Kwanza ya Ulimwengu. Wao hawazitangazi habari njema kwamba ufalme wa Kimasihi mikononi mwa Bwana Yesu ulizaliwa mbinguni wakati Majira ya Mataifa yalipomalizika katika mwaka wa 1914 wala kwamba ufalme wake wa kimbinguni hauna lo lote la kushughulika pamoja na Ushirika wa Mataifa au Umoja wa Mataifa, ambao Kristendomu anautegemea kwa kuiendeleza amani ya ulimwengu na usalama. Siyo kwa Kristendomu, bali ni kwa mabaki waliotiwa mafuta wa mashahidi wa Yehova wa Kikristo sifa imepaswa kupewa kwa ajili ya kuhubiriwa kwa habari njema pote palipo na kuumba kwa ufalme huo wa Kimasihi kama ulivyosimamishwa sasa katika mbingu tangu mwaka wa 1914 kwa ajili ya kukuondosha kuumba kote kwa kidunia kwa uovu wote na kwa ajili ya kuwabariki wanadamu na serikali kamilifu, ya kimungu.
13. (a) Mabaki waliotiwa mafuta walipotokea kutoka Vita ya Kwanza ya Ulimwengu, wafuasi wa Ufalme uliozaliwa karibuni walikuwa wengi kadiri gani, na kwa sababu gani? (b) Mabaki hawa walipataje kuwa na “mina” za mfano, nao walifanyaje biashara nazo?
13 Wakati mabaki hao waliotiwa mafuta walipotokea katika Vita ya Kwanza ya Ulimwengu na mateso yake katika mwaka wa 1918, walikuwa chombo cha chuki ya mataifa yote nao walikuwa chini ya sifa mbaya kwa kidini. (Mt. 24:9) Shamba lililositawishwa walilobaki nalo kwa ajili ya kutokeza wafuasi zaidi wa ufalme wa Mungu wa Kimasihi uliozaliwa upya lilikuwa dogo sana. Wao walikuwa kama mitume na wanafunzi wenzi wake Kristo kati ya ufufuo wa Bwana Yesu kutoka kifo cha aibu na sikukuu ya Pentekoste. Kwa hiyo kilichotukia kilikuwa kama kukabidhiwa kupya kwa mina za fedha za mfano katika mwaka wa 1919 kwa mabaki waliotiwa mafuta wa mashahidi wa Yehova wa Kikristo. Katika mwaka huo, 1919, lilikuja kusanyiko kubwa la kwanza lililofuata vita la mabaki waliotiwa mafuta, katika Cedar Point, Ohio, na, wakifanywa wapya na roho ya Yehova Mungu, mabaki waliotiwa mafuta walijipanga upya kufanya biashara na mina za fedha za mfano zilizopokewa upya kutoka kwa Bwana Yesu sasa aliyevikwa uwezo wa kifalme. Katika njia yao ya kufanya biashara na “mina” hizo, waliuiga mfano wa mitume wa karne ya kwanza kwa kuzihubiri na kuzifundisha “habari njema hizi za ufalme.”—Mt. 24:14, NW.
14, 15. (a) Ni akina nani sasa wanaoitwa watoe hesabu juu ya namna walivyozitumia “mina”? (b) Katika mfano, zawadi za watumwa waliompatia Bwana wao utajiri zilikuwa nini?
14 Sasa washiriki wa mabaki waliotiwa mafuta wanaitwa kutoa hesabu juu ya namna ambavyo wamezitumia mina za mfano. Wao wanajua kwamba ongezeko linatazamiwa kwao na Bwana wao. N’nini thawabu ya kuiongezea hesabu ya mina za mfano? Mfano wa Yesu, alipokwisha kusimulia hesabu iliyotolewa na mtumwa aliyepata faida ya mina kumi zaidi, unaendelea kulijibu ulizo hili:
15 “Kwa hiyo yeye [Bwana aliyerudi] akamwambia, ‘Vema, mtumwa mwema! Kwa maana katika jambo dogo sana umejionyesha kuwa mwaminifu, na uwe na mamlaka juu ya miji kumi.’ Halafu [mtumwa] wa pili akaja, akisema, ‘Mina yako, Bwana, ilifanyiza mina tano.’ Akamwambia huyu vile vile, ‘Nawe, pia, usimamie miji mitano.’”—Luka 19:17-19, NW.
16. (a) Uhakika wa kwamba “kabaila” aliweza kuwapa watumwa wawili kati ya wale kumi utawala juu ya miji kumi na mitano, waonyesha nini? (b) Kwa habari ya washiriki wa mabaki ambao sasa wanampatia Bwana Yesu Kristo aliyerudi utajiri, namna gani juu ya kupata kwao utawala sasa duniani juu ya miji?
16 Uhakika wa kwamba “kabaila” aliyerudi angeweza kuwaweka watumwa wema na waaminifu walioleta ongezeko watawale miji, mtumwa mmoja miji kumi na yule mwingine mitano, wahakikisha kwamba alikuwa amejipatia uwezo wa kifalme naye sasa alikuwa akiutumia. Kuweza kwa kabaila kuwaweka watumwa juu ya miji kumi na mitano, katika habari ya wawili wa kwanza, kwaonyesha kwamba uwezo wake wa kifalme ulikuwa mwingi sana. Kwa maana walikuwa wamekuwa waaminifu wakiwa na hesabu ndogo kwa kulinganisha kama mina ya fedha, wangeweza kukabidhiwa madaraka zaidi, utawala juu ya miji. Katika utimizo wa siku hizi wa mfano, wale wa mabaki waliotiwa mafuta wanaoviongeza vitu vyenye thamani vya Bwana Yesu Kristo anayetawala wakati huu wanacho kibali chake kwa sasa. Wanaendelea kuwa na tumaini lao la utawala pamoja naye katika ufalme wa kimbinguni. Lakini kwa sasa, mnamo utumishi wao wenye bidii duniani, hawapewi utawala wo wote halisi juu ya hesabu ya miji ya kidunia. Kibali cha Bwana wao kingali hakiwapi mamlaka ya kuchezacheza katika siasa za ulimwengu wala kupata utawala wa kisiasa duniani. Lazima waendelee kuwa wasio sehemu ya ulimwengu huu hata kufa ili wakatawale na Kristo juu.
“MTUMWA MWOVU”
17. Ni ulizo gani linalotokea juu ya kuona uchungu kwa mtu kwa sababu ya kutakiwa amletee Bwana ongezeko, na ni kisa gani cha kuona uchungu kinachoonyeshwa na mfano wa Yesu?
17 Je! ye yote kati yetu anaona uchungu juu ya uhakika wa kwamba Bwana Yesu Kristo, sasa akiwa amevikwa uwezo wa kifalme, anahitaji ongezeko juu ya anachowakabidhi watumwa wake? Kama tunastahili kusamehewa kwa kuona hivyo juu yake yaonyeshwa katika habari ya mtumwa aliyetofautiana na wale waliojishughulisha na mina zao. Twasoma: “Lakini mwingine akaja, akisema, ‘Bwana, mina yako hii, niliyoiweka mbali katika kitambaa. Wajua, mimi nilikuogopa wewe, kwa maana wewe ni mwanamume mkatili; wewe huchukua kile usichokiweka na kuvuna usichokipanda.’”—Luka 19:20, 21, NW.
18. Kwa nini mtumwa huyu asiye na faida hakupaswa kusamehewa kwa sababu ya dhamiri?
18 Je! mtumwa huyu aliye tofauti alipaswa kusamehewa kwa sababu ya dhamiri? Hapana; kwa maana yeye hakuombwa kufanya kosa, yaani, kuitumia mina ya Bwana wake katika kupata faida ya udhalimu. Bila ya kujali maoni yake juu ya bwana wake, yeye alikuwa mtumwa tu na ingalimpasa kufanya jambo la uaminifu ambalo bwana wake alimwomba kufanya. Ikiwa alikuwa mvivu mno asiweze kufanya kazi, ingalimpasa kuiweka mina katika benki na kuwaacha wafanya kazi wa benki wamfanyie kazi. Kwa hiyo yeye alikuwa nao udhuru usiofaa kitu.
19. Bwana alimjibu mtumwa huyu kulingana na nini, na namna gani?
19 Bwana wake alimjibu na kumhukumu kulingana na udhuru wake mwenyewe, maana twasoma: “Akamwambia, ‘Kutoka kinywani mwako mwenyewe mimi nakuhukumu, mtumwa mwovu. Wewe ulijua, sivyo, kwamba mimi mwanamume mkatili, nikichukua nisichokiweka na kuvuna nisichokipanda? Basi mbona hukuiweka fedha yangu katika benki? Ndipo wakati ambapo ningerudi ningaliichukua ikiwa na faida.”—Luka 19:22, 23, NW.
20, 21. (a) Kuitwa kwa mtumwa “mwovu” na bwana lilikuwa jambo lisilofaa, la ukatili, la kutokumfikiria huyo? (b) Mfano waonyesha nini juu ya kama “mtumwa mwovu” alistahili nafasi nyingine?
20 Kumwita mtumwa wake aliye goigoi “mwovu” halikuwa jambo lisilofaa, la ukatili na la kutomfikiria huyo kwa kufaa, kwa maana mtumwa huyu aliyeogopa kufanya kazi na mina yenye thamani ya bwana wake alikuwa amemletea bwana wake hasara kwa makusudi. Wakati wenye thamani na fedha ‘vilitiwa ndani, naye mtumwa huyo hakuwa amevitumia kwa uaminifu kwa bwana wake au kwa tamaa ya ufanisi na ongezeko la mali za bwana wake. Kurudisha kwa mtumwa kile tu alichokuwa amepokea wakati mwingi uliopita haikuwa njia nzuri kwa mtumwa kumpokea mfalme nyumbani! Lo! ilikuwa ovyo kama nini! Lo! yenye dharau kama nini! Lo! namna isivyo na adabu! Lo! ukosefu huo wa furaha na shauku juu ya ufalme uliosimamishwa karibuni wa bwana wake! Huku kulikuwa ni kushindwa kabisa kumtolea bwana wake utumishi wo wote na hali alikuwa nao wakati na njia ya kufanya hivyo. Wakati wa kukata maneno, je! yeye alistahili nafasi zaidi? Angalia:
21 “Kisha yeye [bwana] akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu, ‘Mnyang’anyeni mina ile na kumpa yeye aliye na mina kumi.’ Lakini wao wakamwambia, ‘Bwana, huyo anazo mina kumi!’—‘Mimi nawaambieni, Kwa kila mtu aliye nazo, zaidi zitatolewa; lakini kutoka kwa yeye asiye nazo, hata ile aliyo nayo itachukuliwa. Zaidi ya hayo, adui zangu hawa wasionitaka mimi niwe mfalme juu yao waleteni hapa nanyi mwachinje mbele yangu.’”—Luka 19:24-27, NW.
22. (a) Hivyo ni nafasi gani ya kifalme aliyoipoteza mtumwa huyo asiye na faida? (b) Kwa kweli mtumwa huyo alijiweka katika upande wa nani, nayo maneno ya bwana wake yalifanyaje uelekee kuwa msiba kwa mtumwa huyo?
22 Kuchukuliwa kwa mina kutoka kwa mtumwa asiye na faida kulimaanisha kwamba yeye aliipoteza nafasi yake ya kujionyesha mwenyewe kuwa anayestahili ‘kuwa na mamlaka juu ya miji kumi’ na ‘kusimamia miji mitano’ na hivyo kushiriki katika ufalme wa bwana wake aliye mwenye fahari sasa. (Luka 19:17, 19, NW) Asingeweza kukabidhiwa madaraka yo yote ya Ufalme. Ajapokuwa alikuwa na nia iliyo tofauti kuelekea ufalme wa bwana wake, yeye alijiweka katika upande wa wale wenye nia ile ile ya kutokumtaka mwanamume huyu awatawale kama mfalme. Kama aliuawa pamoja na adui za bwana wasiomtaka awe mfalme juu yao, mfano hausemi wala kuonyesha. Lakini mfano waonyesha kwamba mara tu bwana anapomaliza kusema mtumwa asiye na bidii wala asiyependezwa na ufalme wa bwana wake atanyang’anywa nafasi yo yote aliyo nayo, bwana anawaambia raia zake za kifalme kuwachinja adui zake mbele yake.
23. (a) Mtumwa huyo hakuaibishwa kama “mwovu” kwa sababu ya matendo gani mapotovu? (b) Kwa kukumbuka kushindwa kwa mtumwa huyo, “watumwa” wa Kristo waliobatizwa na wakatiwa mafuta wana wajibu wa kufanya nini tangu mwisho wa Majira ya Mataifa katika mwaka wa 1914?
23 Yapaswa iangaliwe kwamba mtumwa huyu asiye na faida hakuaibishwa kama “mwovu” kwa sababu ya kuwatukana watumwa wenzake wala kwa kuwa alifanya ufisadi kama vile uasherati, uzinzi ama kumlala mwanamume mwenzake. Sivyo, bali alihukumiwa kama mwovu kwa sababu ya ukosefu wake wa kutokuyategemeza matumaini ya Ufalme ya bwana wake, kutokufanya kazi kwake kwa ajili ya ongezeko la utajiri wa ufalme wa bwana wake. Kwa kutokuwa upande wa bwana wake kama mfalme, alikuwa akimpinga. (Mt. 12:30; Luka 11:23) Kwa hiyo, vile vile, tangu mwisho wa Majira ya Mataifa katika mwaka wa 1914, ni jambo zito kwa “watumwa” waliobatizwa na kutiwa mafuta wa Mfalme Yesu Kristo anayetawala sasa kuupuza wajibu wao wa kuuongezea ujuzi wa waziwazi, tegemezo na ufuasi wa uaminifu kwa ufalme wake. Wao wamewekewa wajibu wa ‘kufanya biashara’ na mina za mfano walizokabidhiwa wazitumie mpaka atakapofanya hesabu nao.
24. (a) Ni pendeleo gani ambalo “watumwa” hawa wa Kikristo hawataki litolewe kwao apewe mtu mwingine? (b) Kupoteza kwao zawadi ya kifalme kungemaanisha kupoteza nini?
24 Haiwapasi kutaka mapendeleo yao kwa habari ya ufalme wake Kristo yaondolewe kutoka kwao na kupewa kwa mhubiri na mwalimu wa Ufalme mwenye bidii kama yule mtumwa aliyepata faida ya mina kumi. Kunyang’anywa kwao mina ya mfano kungewamaanishia kupoteza mahali katika Ufalme wa kimbinguni, kutawala, kana kwamba ilikuwa, juu ya “miji kumi” au “miji mitano.” Kupoteza kwao hilo kungemaanisha kupoteza vyote. Kungemaanisha uharibifu wao pamoja na adui za moja kwa moja za serikali ya Mungu ya Kimasihi wasiomtaka Yesu Kristo atumie uwezo wa kifalme juu yao kwa miaka elfu. (Ufu. 20:4, 6) Wakati wa malaika watakatifu watakaofuatana na Yesu Kristo katika kuja kwake kukitekeleza kisasi cha kimungu juu ya wapinzani wote na wasiouunga mkono ufalme wa Kimasihi unakaribia. Utaanza mbele ya pigano la Har–Magedoni.
25. (a) Kwa sababu gani kutekelezwa kwa kisasi cha kimungu kutaanza mbele ya pigano la Har–Magedoni? (b) Kwa hiyo basi itamaanisha nini kwetu ikiwa, kama Wakristo wa kujidai, twapatikana tukiwa kama yule “mtumwa mwovu”?
25 Utaanza na uharibifu wa Babeli Mkuu wa kidini mwanzoni mwa “dhiki kubwa” iliyofananishwa na mazingiwa na uharibifu wa Yerusalemu nyuma huko katika mwaka wa 70 C.E. (Ufu. 17:1-16; Mt. 24:15-22) Ole wetu basi iwapo tumo katika jamii hiyo ya Wakristo wa kujidai waliofananishwa na “mtumwa mwovu” aliyeihifadhi mina yake katika kitambaa akaja kuipoteza tu mwishowe! Itamaanisha uharibifu wa milele kwetu katika “dhiki kubwa” pamoja na “adui” zake Mfalme.
26. Ni jamii gani mbili zitakazookolewa zisichinjwe pamoja na adui za Mfalme? Na kwa sababu gani?
26 “Watumwa” waliotiwa mafuta wa Kikristo wanaomletea Bwana wao wa kimbinguni faida ya kiroho, Mfalme Yesu Kristo, wataokolewa wasiuawe pamoja na adui zake Mfalme. Ndivyo na “mkutano mkubwa” wanaouitikia utendaji wa biashara wa “watumwa” wenye faida walio waaminifu na wanaosimama mbele za kiti cha enzi cha Yehova Mungu na cha Mwana-Kondoo wake Yesu Kristo na wanaopiga kelele kwa shauku kusudi wote wapate kusikia: “Ushindi ni kwa Mungu wetu anayeketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo!”—Ufu. 7:9, 10, 14, 15, NE.