Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 10/1 uku. 453
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Matata ya Useja
  • Je, Useja wa Kidini Ni Takwa kwa Wahudumu Wakristo?
    Amkeni!—1998
  • Je, Useja ni Takwa la Wahudumu Wakristo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Je! kwa Kweli Twahitaji Makuhani?
    Amkeni!—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 10/1 uku. 453

Ufahamu Katika Habari

Matata ya Useja

● Amri ya karne nyingi ya useja kwa mapadre wa Kikatoliki inaleta matata kwa mara nyingine.

Si ajabu kwamba inafanya hivyo. Takwa hilo linapingana moja kwa moja na mafundisho ya Biblia.

Siku ya Desemba 23, gazeti la Vatican “L’Osservatore Romano,” likiwasihi mapadre wasiache huduma yao, lilisema kwamba lazima kila padre “afanye lisilowezekana aweze kubaki katika cheo chake.” Takwa hilo “lisilowezekana” kwa kweli latokana na kuanguka na kuiacha ibada ya kweli kulikoanza baada ya kufa kwa mitume wa Yesu Kristo. Mtume Paulo alitabiri kwamba mojawapo ya sehemu za ukafiri huo ingekuwa ‘kuzuia watu wasioe.’ Je! hiyo inakushangaza? Angalia mwenyewe katika tafsiri yo yote ya Biblia, katika 1 Timotheo 4:1-3. Kwa wazi Kanisa la Katoliki limeiacha kanuni ya Biblia kwa kuipendelea yake lenyewe, na hii yaleta matata.

Makala katika “L’Osservatore” iliendelea kuwaambia wale ambao ni mapadre hivi: “Ukitenda makosa ya ufisadi​—haikupasi kufanya hivyo, lakini huenda ikawa hivyo, kwa maana u dhaifu mno​—⁠una vitulizo vingi.” Kulingana na “Newsweek” (Desemba 3, 1973), mapadre wengine wanatafuta ‘kitulizo’ chao wenyewe kwa kushirikiana sana na wanawake na, nyakati nyingine, kwa kufanya ngono nao wajapokuwa wanaendelea kutooa.

Bila shaka, hilo si jambo jipya. Wakatoliki wengi wamejua mapadre wanaofanya hivyo kwa muda mrefu. Lakini kinachohangaisha kanisa siyo ufisadi wa mapadre hawa, bali uhakika wa kwamba wengi sasa wanaacha upadre wakaoe. Hesabu ya mapadre imepungua kwa kiasi cha karibu 20,000 miaka mitatu iliyopita.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki