Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 9/15 kur. 427-428
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Choyo Chatawala
  • Hofu ya Uhalifu
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 9/15 kur. 427-428

Ufahamu Katika Habari

Choyo Chatawala

● Mafundi katika mataifa yenye kutumia madini sana wanaona shida ikija, kuongezeka sana kwa bei ya madini yaliyo ya muhimu.

Afisa mmoja anatetea kukusanya vifaa akibani ili waweze kufanya maafikiano wanaposhughulika na nchi zenye kufanyiza madini. Akasema, “Msiwaache maharamia hawa wawazuie katika jambo hili.”

Sababu hasa ya wasiwasi ni kwamba mataifa yanayogawa madini ya aluminium ore yanapanga kuanzisha tengenezo linalofanana na lile la nchi zinazopeleka mafuta katika nchi nyingine (Organization of Oil Exporting countries), ambalo lilipandisha bei za mafuta kwa kadiri ya juu sana. Matengenezo mengine ya nchi zenye shaba na bati yamekwisha tokea.

Kuyaita mataifa yenye madini haya “maharamia” hakufai kwa maana yafaa kuona makosa ya mtu mwenyewe kabla hajaweza kuyaona ya mwenzake. Fikiria hali ya mataifa hayo. Wafanya kazi katika mengi ya mataifa hayo wameishi wakiwa na mshahara mdogo sana. Nao wanakumbuka vile vile namna ambavyo mataifa yaliyotajirika zaidi yalivyowatumia mara nyingi kwa faida yao yenyewe.

Hali hii ni ushuhuda mwingine wa kwamba hali ya uchumi ya ulimwengu huu imejawa na choyo. Choyo chatawala.

Kwa kweli, shida hizi ni ishara za kwamba hii taratibu iliyopo karibuni itaondoshwa na ufalme wa Mungu. Nabii wa Mungu asema, chini ya utawala wake “haki ndiyo watakayojifunza wakaaji wa nchi yenye mazao bila shaka.” Hilo litakuwa badiliko lenye kufurahisha sana!​—Isa. 26:9, NW.

Hofu ya Uhalifu

● Hofu inapenya katika “sehemu zote za jamii ya United States,” kulingana na hesabu ya watu waliohusika iliyochukuliwa mwaka wa 1973. Mtu mmoja kati ya watu watatu katika miji mikubwa na mmoja kati ya watu watano vitongojini ameshambuliwa na wanyang’anyi, au akaibiwa nyumbani kwake au mali yake ikaharibiwa ovyo ovyo mwaka uliopita. Watu wanne kati ya watu kumi wanaogopa kutembea peke yao usiku hata katika ujirani wao wenyewe.

Watu wengine wanadhani kwamba njia ya kupambana na jeuri ni kuwa tayari kufanya jeuri nawe unapofanyiwa. Kama matokeo, katika Detroit, ambao ndio mji wenye uhalifu mwingi zaidi katika taifa, imekadiriwa kwamba kuna bunduki 500,000, moja ikiwa ya mtu mmoja kati ya watu watatu, mwanamume, mwanamke na mtoto. Hali hii si tofauti sana mahali pengine. Watu wanaishi kwa hofu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki