Kufundisha Mwalimu
● Msichana mwenye umri wa miaka kumi na mitatu katika Netherlands alikutana na mwalimu wake wa somo la biology (linalohusu habari za maisha ya watu, wanyama na mimea) akamwachia kitabu Did Man Get Here by Evolution or by Creation?, alipokuwa akitembelea watu nyumbani kwao kushiriki kweli za Biblia pamoja nao. Baada ya hapo, msichana huyu akawa akijifunza na mwalimu wake (wa kiume) kitabu hiki katika pembe yenye utulivu ya mahali pa kulia chakula shuleni wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana. Kwa sababu hiyo, mwalimu huyo wa biology mwenye umri wa miaka 50 akaacha kuunga mkono wazo la mageuzi.