Nuru ya Kweli Yaangaza Katika Afrika Mashariki
MWAKA wa 1931, shamba kubwa mno katika Afrika, lile la Afrika Mashariki nchi zilizotawalwa na Waingereza, lilianzwa. Afrika Mashariki ndizo zile nchi tatu, Kenya, Uganda na Tanzania (Tanganyika na kisiwa cha Unguja.) Katika miaka ya mapema kuanzia na mwaka wa 1930 nchi hizi zote zilikuwa chini ya mamlaka ya Uingereza. Kwa vile kulitokea roho ya kutaka kujitawala katika Afrika, kila moja ya nchi hizi ikajipatia uhuru wake kutoka Uingereza. Mwaka wa 1962, nchi ya Tanganyika ikajipatia uhuru na kuwa jamhuri ya Tanzania katika Jumuiya ya Madola ya Uingereza. Mwaka ule ule nchi ya Uganda ikajipatia uhuru wake, na Kenya mwaka wa 1963. Kwa sababu ya mataifa na makabila mengi ya watu wanaoishi katika sehemu hizi, kuna tatizo la lugha nyingi, lakini Kiswahili ni lugha inayotumiwa na wote katika Afrika Mashariki yote.
Kidini, mtajo huu “Afrika Yenye Giza” umefaa sana. Wingi wa wenyeji wamekuwa wafuasi wa dini za kipagani. Kwa miaka mingi misheni za Jumuiya ya Wakristo, za Kikatoliki na za Kiprotestanti pia zimekuwa zikitenda, lakini kama vile mahali pengine katika Afrika, misheni hizi zimeshindwa kutokeza Wakristo ‘wanaoabudu katika roho na kweli.’ (Yohana 4:24) Lakini ulikuwa wakati gani miale ya kwanza ya nuru ilipoanza kuangaza katika sehemu hii yenye giza kiroho ya dunia.
Karibu wakati huu huko Cape Town, Afrika ya Kusini, ndugu aitwaye Gray Smith alikuwa akishiriki utumishi wa upainia-msaidizi. Kaka yake Frank alikuwa ndiye wa kwanza kupata kweli, lakini Gray pia alianza kujifunza kwa uzito mwaka wa 1928. Alibatizwa mwaka wa 1929 na mara akaanza kazi ya upainia msaidizi. Mwishowe, aliungana na Frank katika safari yenye kupendeza sana kuelekea Afrika Mashariki.
Mwaka wa 1931, wote wawili walipelekwa Kenya wakaone kama inawezekana kueneza habari njema katika Afrika ya Mashariki. Wakati huo Kenya ilikuwa sehemu ya utawala wa Uingereza ikiwa na wakaaji karibu 4,000,000, kati ya hesabu hii Wazungu wakiwa 25,000. Walichukua gari, walilofanya kuwa gari la safari, wakasafiri kwa meli iitwayo “Saxon Castle” kuelekea Mombasa, bandari ya Kenya. Toka huko walisafiri na gari lao maili 40 (kama kilometre 600) mpaka Nairobi, mji mkuu wa Kenya, walikokuwa wamepeleka vibweta 40 vya vitabu. Iliwachukua siku nane wafike, kwa sababu ya barabara kuwa mbaya. Walienea Nairobi yote wakaangusha vitabu vyote kwa muda wa kama mwezi mmoja. Vitabu vingi viliangushwa kwa Magoani, Wahindi, lakini vingi vya vitabu hivi vilikusanywa na mapadre wa Kikatoliki vikachomwa moto.
Katika safari yao ya kurudi Afrika ya Kusini ndugu hawa wote wawili walipatwa na ugonjwa wa mbu (malaria). Siku hizo huu ulikuwa ndio ugonjwa mbaya sana. Wakapanda meli iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam, lakini wakawa wagonjwa sana na kuweweseka hata walipofika Durban walitolewa wakapelekwa hospitalini. Frank Smith hakuweza kupona ugonjwa huu, akafa. Gray Smith alipona na ikawa lazima akae miezi minne hospitalini. Walakini, kuelekea mwisho wa mwaka wa 1931 alirudi Cape Town.
Wakati kama huu, huko Uingereza, kijana aitwaye Robert Nisbet akawa ndiyo ameacha kazi nzuri katika idara ya kutengenezea dawa huko London na alikuwa tayari kuanza utumishi wa upainia. Ndugu Rutherford, ambaye wakati huo alikuwa huko London, alimpelekea barua akisema: “Tunatafuta mtu wa kwenda Cape Town; ungependa kwenda?” Robert alikubali na mara akaanza kufunga safari.
Alipofika kwenye afisi ya Cape Town, Ndugu Nisbet alionyeshwa mzigo mwingine wa vitabu uliokuwa ukingojea kutumwa Afrika Mashariki, wakati huu vilikuwa vibweta (cartons) 200! Alisikia habari za safari ya akina ndugu Smith na msiba uliompata Frank. Ijapokuwa hivyo, aliukubali mgawo wa kwenda Afrika Mashariki kwa shauku. David Norman akajiunga naye, wakasafiri kuelekea mgawo wao. Iliwapasa kuhubiri maeneo yote ya Kenya, Uganda, Tanganyika na Unguja—shamba kubwa mno kweli kweli!
Wakijilinda juu ya ugonjwa wa mbu kwa kutumia vyandalua wakati wa kulala na kutumia kwinini (dawa ya kuzuia ugonjwa wa mbu) kwa wingi, iliyopatikana katika afisi zote za posta katika Afrika Mashariki kwa kununuliwa, na vilevile kuvaa kofia za kujilinda na jua kali mchana, walianza shughuli yao ya kuhubiri Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanganyika, Agosti 31, 1931. Kama inavyoonyeshwa na maelezo ya Ndugu Nisbet huu haukuwa mgawo rahisi: ‘Jua kali lililong’aa katika barabara, fukuto (jasho au joto) jingi lenye kunata na uhitaji wa kuchukua mizigo mizito sana ya vitabu nyumba kwa nyumba ilikuwa baadhi ya matatizo tuliyopaswa kuyapata. Lakini tulikuwa vijana na wenye nguvu tukafurahia.’
Katika muda wa juma mbili mapainia hawa wenye juhudi wakawa wameangusha vitabu vikubwa na vidogo vyapata elfu moja, kati ya vitabu hivyo vilikuwako vitabu vilivyoitwa “Rainbow Sets,” kwa sababu vilikuwa vitabu vyenye rangi mbali-mbali. Jambo hili lilichochea hasira ya mapadre, na taarifa ikawekwa penye ubao wa matangazo wa kanisa la Kikatoliki ikielekeza fikira za Wakatoliki wote kwenye sheria Na. 1399 ya sheria za kanisa zinazokataza Wakatoliki hata wasiwe na vitabu hivyo nyumbani mwao. Vingi vya vitabu hivi viliangushwa kwa Wahindi. Kwa sababu walikuwa hawana vitabu vya Kiswahili na kwa sababu Waafrika hawakuwa na elimu, ndugu hawa hawakuweza kufanya kazi miongoni mwa Waafrika.
Kutoka Dar es Salaam waling’oa nanga wakaelekea Unguja, kisiwa chenye umbali wapata maili 20 (kilometre kama 32) kutoka mwambao (pwani au bara), ambacho zamani kilikuwa kituo cha kuuzia na kununua watumwa. Mji huu wenye barabara ndogo zenye kupotoka-potoka, ambamo ni rahisi mgeni kupotea, ulienezwa na harufu nzuri ya karafuu, maana Unguja hupatia karibu ulimwengu wote karafuu. Ulikuwa na robo milioni ya wakaaji, ambao kama 300 walikuwa Wazungu—waliokuwa watawala wakati huo. Wengi sana walikuwa Waswahili na karibu 45,000 walikuwa Wahindi na Waarabu. Vitabu vingi viliangushwa kwa Wahindi hawa na vingine kwa Waarabu. lakini tena kwa vile wakaaji wengi sana walikuwa Waswahili, hawakuweza kufikiwa kwa ujumbe wa Ufalme.
Walipokwisha kukaa siku kumi Unguja, wakapanda meli kuelekea Mombasa, bandari ya Kenya, mpaka bara za Kenya, wakiwa na mboga na matunda mengi. Wakasafiri kwa gari la moshi na kuihubiri miji ya kando ya njia ya reli kuelekea Ziwa Victoria. Walivuka ziwa hili, mwendo wa maili 250 urefu na maili 150 katika upana, kufika Kampala, mji mkuu wa Uganda. Wakagawa vitabu vingi huku na kupata maandikisho ya gazeti The Golden Age. Jamaa mmoja alitoka maili 50 kichakani akamwona rafiki yake akisoma kitabu Government kwa shauku sana. Alifika Kampala kwenda kuwatafuta vijana waliokuwa wakigawa kitabu hiki. Alichukua nakala ya vitabu vyote akaandikisha gazeti The Golden Age.
Kabla ya kuanza safari yao ya kurudi kwa njia ya gari walitembea mji mwingine maili 25 ndani ndani ya nchi, wakafurahi sana kwa vile wametumiwa kuupeleka ujumbe wa Ufalme kwa mara ya kwanza kwa njia ya vitabu katika sehemu ya ndani ndani ya Afrika. Wakarudi kutoka mji huu wakipita njia nyingine wakawa wamepata maono yenye kufurahisha ya kutembelea poromoko la maji liitwalo Ripon Falls, chanzo cha Mto Nile. Walipokuwa wakirudi kwenda Mombasa walihubiri miji mingine michache kando ya njia ya reli. Wakiisha kuhubiri Mombasa katika joto jingi mno, wakiangusha vitabu vingi na kutoa hotuba mbili zilizohudhuriwa na watu wengi, walikwenda mahali pengine kando ya pwani kisha, walipopanda meli inayoitwa “Llandovery Castle,” wakarudi Cape Town, Afrika ya Kusini, safari ya maili 3,000.
Katika safari hizi mbili za kwanza kuingia Afrika Mashariki vitabu vikubwa na vidogo zaidi ya 7,000 viliagushwa na kupatikana maandikisho mengi ya The Golden Age. Bila shaka sehemu ya mbegu hizi iliangukia udongo mzuri, kwa maana jamaa mmoja aliyekuwa amepokea vijitabu aliiandikia Sosaiti katika Cape Town akaagiza aina yote ya vitabu vikubwa na vidogo vya Judge Rutherford. Alikuwa msimamizi wa shimo la dhahabu katika eneo la bundu Tanganyika. Basi kwa gharama kubwa ya fedha, jitihada na hata uhai wenyewe upande wa mapainia wenye kujitoa na wenye bidii, ule ujumbe ulikuwa ukiingia Afrika Mashariki ya utawala wa Waingereza na kazi ya Ufalme ilikuwa ikiendelea.
Ndiyo, mwaka wa 1931 shamba kubwa lilifikiwa na waaminifu wachache wakati huo katika Afrika ya Kusini. Mwaka huo jumla ya vitabu 68,280 viliangushwa katika Afrika ya Kusini na makusanyiko nane yalifanywa ili kuitia nguvu imani ya ndugu.
JITIHADA MPYA KATIKA AFRIKA MASHARIKI YA UTAWALA WA UINGEREZA
Kama ilivyotangulia kutajwa, Afrika Mashariki ya utawala wa Uingereza ilitembelewa na Ndugu Gray na Frank Smith mwaka wa 1931, na baadaye na Robert Nisbet na David Norman. Wakati wa ziara hizi vitabu vingi viliangushwa na ushuhuda mkubwa ulitolewa. Lakini ulifika wakati wa ziara nyingine.
Shughuli ya tatu ya kuingia katika Afrika Mashariki ilifanywa na mapainia wanne kutoka Afrika ya Kusini mwaka wa 1935. Walikuwa Gray Smith, mkewe na ndugu wawili, Robert na George Nisbet. Wakati huu walikuwa wamejitayarisha sana wakiwa na motokaa mbili zenye uzito wa robo tatu zenye mahali pa kulala, vitanda kamili, jiko, maji na tangi ya ziada ya petroli, vilevile chandalua cha kujilinda na mbu. Mpango huu uliwawezesha kufikia mahali ambapo zamani hapakuwa pamehubiriwa, ijapokuwa barabara zilikuwa zimemelea majani mpaka futi kumi kwenda juu. Mara nyingi walilala misituni na waliweza kuona, kusikia na kujua hali ya Afrika ilivyokuwa ikiwa na wingi wa wanyama—simba wenye kunguruma usiku, punda milia wanaokula kwa amani, twiga na kifaru na tembo.
Walipofika Tanganyika walitengana. Ndugu Smith na mkewe walibaki Tanganyika kwa muda, hali akina Nisbet waliendelea Nairobi, ambako walikutana baadaye na akina Smith. Walipokuwa Tanganyika akina Smith walikamatwa wakaamriwa warudi Afrika ya Kusini. Lakini Ndugu Smith aliamua kuendelea Nairobi kwa vile alivyokuwa na paspoti ya Afrika ya Kusini iliyokuwa imeandikwa “raia wa Uingereza kwa kuzaliwa.” Wakati wa kufika Nairobi, Kenya, yeye na mkewe walikwenda mara hiyo kwa wakuu wa polisi wakaombe ruhusa ya kukaa, wakiweka dhamana ya shilingi 2,000/-ambazo walirudishiwa waliporudi kusini.
Wakaendelea Uganda. Walipofika Kampala, wakaona ni mahali penye uadui ambapo polisi waliendelea kuwachunguza. Hata hivyo waliweza kuangusha vitabu vingi kabla ya kulazimishwa kuondoka Uganda kwa sababu ya kufukuzwa kwa amri ya gavana. Basi wakasafiri kurudi Nairobi, walikoungana tena na akina Nisbet.
Huku, pia, walipata upinzani kutoka kwa wenye mamlaka, lakini ushuhuda bora ulitolewa, vikiangushwa vitabu zaidi ya nakala 3,000 na karibu vitabu vidogo 7,000 na kupata maandikisho mengi ya The Golden Age. Amri za kufukuzwa zilipingwa sana, lakini wenye mamlaka hawakutoa maelezo yenye kufaa.
Wakati wa shughuli hii Robert Nisbet alipatwa na ugonjwa wa matumboni akabaki katika hospitali ya Nairobi lakini wengine wa kikundi hiki wakaanza kurudi. Ndugu Smith na George Nisbet walijaribu kuingia Unguja, lakini wakanyimwa ruhusa ya kuingilia huko; hivyo walirudi Afrika ya Kusini, Robert Nisbet alipata kupona na hatimaye, katika mwaka wa 1955, akawa ndiye mwangalizi wa kwanza wa tawi la Maurishasi. Nduguye George, alipokwisha kutumikia kwa muda fulani kama mmisionari katika Maurishasi, alirudishwa Afrika ya Kusini akaanza kutumikia mwaka wa 1958 katika tawi la Afrika ya Kusini.
Mapainia hawa waliovumbua njia katika “Afrika Yenye Giza” walikuwa na imani kuu sana ya kupatwa na shida zote na hatari zilizosababishwa na utendaji huu. Kati ya mapainia sita, wanne walikaa siku nyingi hospitalini—kwa sababu ya ugonjwa wa damu katika mkojo, ugonjwa wa mbu na ugonjwa wa matumboni. Kwa jitihada zao vitabu vingi viliangushwa, kuweka msingi wa kazi ya ujenzi wa kiroho ambayo wanafunzi wa Shule ya Gilead walitazamiwa kuianza mwaka wa 1950 na miaka iliyofuata.
NURU YAANGAZA TANGANYIKA
Kaskazini ya mbali, katika Tanganyika, kazi miongoni mwa ndugu Waafrika iliendelea pia. Wakati wa miaka ya tangu mwaka wa 1936 barua kutoka Tanganyika zilizolifikia tawi la Sosaiti la Cape Town zilionyesha kwamba miale ya kweli ilikuwa ikiangaza katika sehemu hii ya Afrika, ijapokuwa ni kwa utusitusi. Mwaka wa 1942, ndugu 158 walishiriki kazi kidogo. Kulingana na Yearbook cha mwaka wa 1945, ripoti kutoka Tanganyika zilionyesha kuongezeka kwa upinzani na kutawaliwa kwa vitabu na serikali, lakini kulikuwako wastani ya kila mwezi ya wahubiri 75 waliokuwa wakiripoti zaidi ya saa 8 za shambani kila mhubiri. Njia peke yake iliyoonekana kuwa nzuri kuwatia moyo ndugu hawa ilikuwa kupitia kwa kuandikiana barua, na Sosaiti ilifanya hivi. Mnamo mwaka wa 1945 karibu wakaaji wa nchi hii 6,000,000 walihubiriwa na makundi matatu tu yaliyoanzishwa yenye wahubiri 144. Kazi yao zaidi ilikuwa ya kuhubiri tu, kufanya ziara za kurudia na mafunzo ya Biblia. Wakati fulani walipokea vitabu kukawa furaha kuu. Walitumia vizuri vitabu hivyo kwa faida ya wote. Mnamo mwaka wa 1946 wakawa wameongezeka kufika wahubiri 227 na makundi 7. Ndugu hawa walipingwa sana na madhehebu za dini ya uongo wakahitaji sana usimamizi wa karibu zaidi na vitabu katika Kiswahili.
Mwaka wa 1948 mtumishi Mwemba anayetembelea ndugu alipelekwa kutoka Northern Rhodesia akatembelee makundi Tanganyika. Alifanya kazi pamoja na makundi nane katika wilaya ya Mbeya, akitia moyo na kujenga ndugu. Kundi jingine moja, lililokuwa mpakani mwa Northern Rhodesia, lilitumikiwa na mtumishi mwingine aliyetumwa kutembelea ndugu. Matokeo yalikuwa yakitokea hata wakuu (machifu) walikuwa wakionyesha kupendezwa na kweli. Vilevile, Tanganyika ikaja kuwa sasa chini ya tawi jipya lililoanzishwa huko Northern Rhodesia. Leo Kenya, Uganda na Tanzania zinasimamiwa na tawi la Sosaiti huko Kenya. Kazi ya Ufalme inaendelea kwa haraka katika eneo hilo na inaletea jina la Yehova heshima nyingi.
—1976 Yearbook.