Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 6/1 uku. 11
  • Je! Wakumbuka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wakumbuka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
  • Habari Zinazolingana
  • Wanefili Walikuwa Nani?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Haraka Inayokupasa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Je! Unakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Je! Wakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 6/1 uku. 11

Je! Wakumbuka?

Umesoma matoleo ya karibuni ya Mnara wa Mlinzi kwa uangalifu? Ikiwa ndivyo, bila shaka utayakumbuka mambo haya:

● Wale waliomsikia Yesu Kristo akisema katika karne ya kwanza W.K. wangewezaje ‘kutoka mautini waingie uzimani’?​—Yohana 5:24.

Kwa sababu walikuwa wenye dhambi, watu wa siku za huduma ya Yesu ya kidunia walikuwa chini ya laana ya mauti. Walakini, kwa kumsikiliza Mwana wa Mungu, kutubia makosa yao na kumkubali kuwa Masihi aliyeahidiwa ambaye angewakomboa kutokana na dhambi na mauti, watu mmoja mmoja walitoka chini ya laana. Hivyo, katika njia ya mfano, ‘walitoka mautini wakaingia uzimani.’​—2/15/ uku. 7.

● Mtume Paulo alimaanisha nini alipoandika, “upendo haupungui neno wakati wo wote”?​—1 Kor. 13:8.

Kama inavyoonekana kutokana na habari inayozunguka, mtume alikuwa akizungumza uhakika wa kwamba upendo utaendelea kuwako, hali karama za miujiza zingekoma. Hivyo, “upendo haupungui neno wakati wo wote” katika maana ya kwamba hautakoma au kupungukiwa.​—⁠3/1 uku. 14.

● Wanafili walikuwa nani?

Katika siku za Noa, walikuwa wazao wa wana wa Mungu wa kiroho waasi na wanawake. Jina Wanefili linamaanisha “Waangushaji,” watu waliowaangusha wengine. Watu hawa wa wazazi wa namna mbalimbali waliongeza sana jeuri iliyokuwako katika siku za Noa.

● Ni nini maana ya uhakika unaoelezwa katika Zaburi 41:3 juu ya Yehova Mungu kubadilisha kitanda cha mwenye haki wakati wa ugonjwa?

Yehova Mungu huwatia watumishi wake nguvu wavumilie ugonjwa na kutia ndani yao tumaini ambalo ni la muhimu katika kuponya ugonjwa. Hivyo Aliye Juu Zaidi hubadilisha kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha kuponyea ugonjwa.​—4/1 uku. 6.

● Sababu gani ni jambo la muhimu kulingana na maoni ya kibinafsi kwamba wanafunzi wa Yesu Kristo wadumishe mwenendo mwema na kuwa na bidii katika kazi ya kutoa ushuhuda hadharani (waziwazi) pamoja na matendo mengine mema?

Bila kujali umri wa mtu ni gani sasa, ama kifo au “dhiki kubwa” itamaliza nafsi yake ya kufanya kumbukumbu la matendo mema pamoja na Yehova Mungu. Kwa hiyo, mtu huyo hapaswi kuwa mzembe katika kutimiza madaraka yake kama Mkristo, kwa kuwa hilo linahusiana na kumbukumbu lake na Muumba wake nalo laweza kuongoza katika kupoteza kibali ya kimungu.​—4/15 uku. 18.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki