Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 2/1 uku. 23
  • Badiliko Kubwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Badiliko Kubwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 2/1 uku. 23

Badiliko Kubwa

Je! nakala moja tu ya gazeti la Kikristo yaweza kweli kuwa na matokeo juu ya mwendo wa maisha ya mtu? Jambo lifuatalo lililoonwa kutoka Spania linaonyesha kwamba yaweza.

Mara nyingi, Roberto mwenye uso wenye hali ya kufikiri anakaa peke yake anapokuwa akisafiri kwa garimoshi, walakini pindi moja alikaa karibu na mwanamume mzee, ambaye alimwuliza: “Je! unapenda kusoma?” Jibu lilikuwa ndiyo, na kwa hiyo Roberto alipewa nakala ya Mnara wa Mlinzi. Ijapokuwa mwanamume huyo mwenye kichwa chenye mvi alishuka akatoka kwenye garimoshi, Roberto aliendelea kusoma mpaka akalimaliza gazeti lote. Alipofika katika kituo cha mwisho cha garimoshi, alisimama katika kituo na kujiuliza: “Unakwenda wapi? Je! huoni kwamba sasa huwezi kufanya ulichokuwa ukitaka kufanya?”

Akiwa hana kazi, na kuwa na deni kubwa na akiwa amekata tamaa, asubuhi hiyo, Roberto asiye na tumaini alikuwa amepanda garimoshi akielekea mji mkuu wa jimbo hilo akiazimia kumwua mtu aliyekuwa akishirikiana naye katika biashara ambaye alikuwa amemdanganya na kumnyang’anya mali yake yote aliyokuwa amejiwekea akiba. Kisha, Roberto alikuwa amepanga kwamba angerudi nyumbani kwake, amwue mkewe na watoto na mwishowe ajiue. Walakini sasa alichukua garimoshi lililofuata akaenda nyumbani kwake, akamwendea jirani yake aliyekuwa Shahidi, akaomba funzo la Biblia.

Baada ya kutafuta-tafuta kwa miezi mingi, Roberto aliyekuwa amebadilika alimwona shahidi wa Yehova aliyekuwa amempatia lile gazeti wakiwa katika garimoshi. Alimwona kati ya kundi la watu katika kusanyiko la Kikristo. Ebu wazia furaha ya mwanamume huyo mzee aliposikia kwamba Roberto pamoja na jamaa yake yote walikuwa wakijifunza Biblia na kuhudhuria mikutano ya watu wa Mungu na kwamba walitazamia kubatizwa karibuni! Ndiyo, gazeti moja lilikuwa limeleta badiliko kubwa!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki