Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 4/15 uku. 24
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • Kitabu Cha Biblia Namba 10—2 Samueli
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Daudi Anafanywa Mfalme
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Soma na Ujifunze Kutokana na Vitabu Viwili vya Mambo ya Nyakati
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Mwenye Nguvu Ingawa Dhaifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 4/15 uku. 24

Maswali kutoka kwa Wasomaji

● Samweli wa pili sura 8:13 inasema kwamba, Daudi aliwaua Waedomi katika Bonde la Chumvi, walakini 1 Nyakati 18:12 inasema tendo hilo lilifanywa na Abishai, na maneno yaliyo kichwa ya Zaburi 60 (NW) yanasema kwamba Yoabu ndiye aliyewashinda. Kwa sababu gani mambo yako hivyo?

Masimulizi hayo matatu kwa wazi yanaeleza kushindwa kwa Waedomi kutokana na maoni matatu tofauti-tofauti. Katika 2 Samweli, inasemekana Daudi ndiye aliyeshinda kwa sababu yeye alikuwa ndiye mfalme, amiri-jeshi wa Israeli na ndiye aliyetoa ruhusa ya kufanya vita. Kwa kuwa Yoabu ndiye aliyekuwa jemadari mkuu, anasifiwa kuwa ndiye aliyeupata ushindi katika maneno yaliyo kichwa ya Zaburi 60 (NW). Abishai alikuwa jemadari wa kikosi kimoja chini ya uongozi wa Yoabu na bila shaka alifanya sehemu kubwa katika shughuli hiyo ya kijeshi. Jambo hilo linaonyesha sababu gani anasemekana ndiye aliyepata ushindi katika masimulizi ya Nyakati. Kwa hiyo hakuna kupingana ko kote. Hata leo ni jambo la kawaida kusema jambo fulani lilitimizwa na yule aliyetoa ruhusa au yule aliyefanya sehemu kubwa katika kulifanya litimie kwa kufanikiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki