Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 5/15 uku. 3
  • Je! Amani Ni Tumaini la Kitambo Tu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Amani Ni Tumaini la Kitambo Tu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Ambavyo Amani Yaweza Kupatikana Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Acha “Amani Ya Mungu” Ilinde Moyo Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Amani ya Kweli—Kutoka Chanzo Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Amani Ambayo Katika Hiyo Umoja wa Ulimwengu Unategemea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 5/15 uku. 3

Je! Amani Ni Tumaini la Kitambo Tu?

AMANI​—imeonwa na watu tangu nyakati za kale kabisa kuwa neno la “kimwujiza.” Hata hivyo ni miaka michache ambayo amani imeenea duniani pote!

Mpaka wakati huu hakuna taifa la ulimwengu lililopata kufaulu katika ‘kufua panga zake ziwe majembe na mikuki yake iwe miundu.’ (Isa. 2:4) Mashindano ya uundaji wa silaha yametumia fedha nyingi sana ambazo zingeweza kutumiwa katika kuleta nafuu (maendeleo) kwa mataifa kiadili na kiuchumi. Kufuata mkataba wa amani ambao Rais Carter wa United States (Amerika) alisaidia kupatanisha kati ya Israeli na Misri, maelezo ya habari na picha yalisema mengi juu ya milundiko mikubwa ya silaha iliyoahidiwa kwa pande zote mbili zenye kuahidi kuwa na “amani.”

Wanafunzi wa jambo hilo wanasema kwamba sababu ya amani kuwa jambo lisilofikilika ni kwa vile inadhaniwa kuwa kuna amani ikiwa tu hakuna vita au mapigano. Makala fulani katika gazeti Sunday Magazine, Oktoba 15, 1978, yenye kichwa “Watu Hawa wa Amani Ni Akina Nani?” ilitoa maelezo haya:

Kuna watu wengine wanaotilia shaka kilipo chama cha amani leo. Kwa mfano, fikiria maoni ya Kasisi Dakt. Homer A. Jack, mwenyekiti wa Baraza ya Matengenezo Yasiyo ya Kiserikali juu ya upunguzaji wa Silaha katika Umoja wa Mataifa.

“‘Hatujapata kuwa na chama cha upunguzaji wa silaha na kwa hakika kumekuwako utendaji mdogo sana wa upunguzaji wa silaha tangu 1964 au 1965,’ akasema. . . . ‘Kila kitu kiliacha kushirikiana kwa sababu ya vita ya Vietnam. Chama cha upunguzaji wa silaha kilivunjika-vunjika, kikatoweka.’ “

“Wengine,” ikasema makala hiyo, “wanashikilia kwamba chama cha kweli cha amani hakipo leo.”

Mtu mwingine mwenye maarifa juu ya jambo hilo, Bw. James H. Laue, ambaye ni msimamizi wa Makao Makuu ya Mafunzo ya Miji Inayokaliwa na Watu wa Namna Nyingi katika chuo kikuu cha Missouri-St. Louis (U.S.A.), na mwenyekiti mwenzi katika Shule ya Shughuli ya Amani ya Kitaifa, alisema juu ya uhitaji wa jitihada za pamoja, ili kufikia amani ya ulimwengu: “Wazo la amani ni zuri, walakini halifahamiki vizuri . . . Jambo ambalo amani imemaanisha kwa miaka mingi sana limekuwa kinyume​—kutokuwapo kwa wasiwasi na mapigano.”

Laue alisema kwamba, tangu mwaka 1935, mapatano 140 yamepitishwa katika Bunge la United States kwa kusudi la kutengeza chuo au shule ya mambo ya amani, walakini wazo la amani wakati wote limeelekea kuwa lisilofahamika vizuri lisiweze kuleta matokeo.

Kama matokeo, kufikia wakati huu amani imekuwa mradi usiofikilika.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki