Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 6/1 uku. 23
  • Ufahamu Katika Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufahamu Katika Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Vichwa vidogo
  • ‘Kuongezeka kwa Uvunjaji wa Sheria Kunapoesha Upendo’
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 6/1 uku. 23

Ufahamu Katika Habari

‘Kuongezeka kwa Uvunjaji wa Sheria Kunapoesha Upendo’

● Vilevile Yesu alitabiri kwamba “kwa sababu ya kuongezeka kwa kutokutii sheria upendo wa wengi zaidi utapoa.” (Mt. 24:12, NW ) Jambo hilo linatokea ulimwenguni pote, sana sana kati ya wale wanaodai kuwa Wakristo, kama ilivyokaziwa na makala ya karibuni katika gazeti “The Wall Street Journal.” Chini ya kichwa Kichwa “Kufufuka kwa Kazi ya kiinjilisti Kunatokea katika Taifa Zima Walakini Kukiwa na Matokeo Machache,” mwandikaji huyo aliandikia maneno haya ya pasta Mbaptisti: “Nilisikia katika mojalapo la maonyesho yale ya kiinjilisti katika TV usiku uliopita kwamba 33% ya Waamerika wote ‘wanazaliwa tena,’ lakini iwapo hiyo ni kweli, sababu gani hesabu ya uhalifu ingali juu sana? Sababu gani dawa za kulevya zingali zinatumiwa sana? Nguvu yetu iko wapi?”

Kuongezeka kwa uvunjaji wa sheria hata katika vyeo vya juu vya jamii kumefanya upendo kwa Mungu na kwa wanadamu wenzetu upoe ambao katika wakati uliopita ulitenda kama kizuizi. Akionyesha njia moja ambayo katika hiyo uvunjaji wa sheria unasitawi, Gilbert Geis, mwalimu mkuu wa uhusiano wa kijamii katika Chuo Kikuu cha California, hivi karibuni alitangaza: “Hesabu iliyo juu zaidi ya uhalifu katika taifa hili i katika Bunge. Riga hesabu ya wanabunge wanaotiwa nguvuni au kufungwa nawe utaona asilimia i juu zaidi ya Mji wa New York.” Matokeo ya hilo, akasema Geis, ambaye anaonwa kuwa mtaalamu wa uhalifu unaofanywa na watu wenye vyeo, ni “wasiwasi katika jamii, kutokutumaini, kutojali na pupa: ‘iwapo wengine wanafanya hivyo, nami pia nitafanya.’ “Hivyo “upendo wa wengi zaidi” unapoa kwa kuwa uvunjaji wa sheria unatokeza uvunjaji wa sheria.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki