Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 2/15 uku. 23
  • Kuhitimu Kwenye Mgawo wa Juu Zaidi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuhitimu Kwenye Mgawo wa Juu Zaidi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Hii Yaweza Kuwa Kazi-Maisha Inayokufaa Zaidi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Watu Wote Wanaalikwa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Maisha Yenye Kuthawabisha Katika Utumishi wa Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Je, Waweza Kujitolea?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2001
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 2/15 uku. 23

Kuhitimu Kwenye Mgawo wa Juu Zaidi

Rafiki wa watu wengi wa mataifa yote, Maxwell G. Friend alikufa Februari 10, 1983, akiwa na umri wa miaka 92. Alizaliwa na wazazi Wayahudi katika Austria, Desemba 7, 1890, na hapo kwanza alikuwa akiitwa Max Freschel. Baada ya kupewa malezi ya dini ya orthodoksi alianza kujifunza Biblia pamoja na Mashahidi Waswisi. Mwishowe akabatizwa Mei 9, 1913, kisha akawa Mwisraeli wa Kikristo aliyepakwa mafuta. Mwaka wa 1914 alitumikia kwenye Betheli ya Ujeremani. Baadaye alipomwoa Irma, wote wawili walitumikia kwenye Betheli ya Uswisi katika Bern. Mwaka wa 1926 walihamishwa wakapelekwa Betheli ya Brooklyn, ambako yeye alibadili jina lake akawa Maxwell G. Friend.a

Katika United States (Amerika) alitumikia akiwa mtafsiri, msemaji mwenye kusafiri na mwelekezaji wa michezo ya kuigizwa ya Kibiblia kwa kutumia kituo cha radio kilichoitwa WBBR. Mwaka wa 1934 akawa mmoja wa walimu waliokuwa wa Shule ya Biblia ya Gileadi huko South Lansing, N.Y. Kwa muda wa miaka 17 alitumikia madarasa 34, akawa mpendwa wa wanafunzi wamisionari zaidi ya 3,600. Alifundisha namna ya Kutoa Hotuba za Biblia kwa Watu Wote na namna ya kufanya Uchunguzi wa Biblia. Wakati wa miaka ya baadaye sauti yake ilijulikana sana na maelfu ya watu katika michezo ya kuigiza mingi ya makusanyiko. Mara nyingi alisema siku moja ‘angehitimu’ afikie mgawo wake wa juu zaidi wa kuwa pamoja na Kristo katika Ufalme wa kimbingu.​—Ufunuo 14:13.

[Maelezo ya Chini]

a Hadithi ya maisha yake imo katika W4/15/67, kurasa 249-255.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki