Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 6/1 uku. 27
  • Mazingira Yasiyo na Mazao kwa Watoto

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazingira Yasiyo na Mazao kwa Watoto
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Ubora wa Kutia Adabu katika Upendo
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Wasaidie Watoto Wako Wasitawi
    Amkeni!—1997
  • Nidhamu Inayofaa
    Amkeni!—2015
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 6/1 uku. 27

Mazingira Yasiyo na Mazao kwa Watoto

POLE KWA POLE jamii ya kisasa imegeuza mazingira yanayofanya mtoto akue akiwa mwenye afya yakawa yasiyoweza kumkuza, anasema Profesa Edward A. Wynne, wa Chuo Kikuu cha Illinois. Yeye analaumu hali ya watu kujifikiria wenyewe mno, kuwa na utajiri, na dini kushindwa kutekeleza wajibu wayo. “Inafahamika ni nini kinachofanya wazazi wengine wajisikie wamezidiwa,” anasema Profesa Wynne katika jarida The Wall Street Journal. “Wengine wanaachilia mambo kwa kushindwa na la kufanya, nao waume na wake waliooana wanapanga kuahirisha au hata kuepuka kulea watoto.” Yeye anashauri njia tofauti zitumiwe, kwa mfano waume na wake waliooana wajitoe kwa uzito ili kulea watoto ifaavyo, na kufanya hivyo huenda kukatia ndani kushirikiana na dini inayotia moyo kuwe na umoja wa jamaa na kutazamia washiriki wayo wajihusishe katika jambo hilo, wakichanganya upendo na nidhamu, na kujinyima miradi ambayo ingaliweza kuwaletea fahari.

Biblia ilikazia uhitaji huo karne nyingi zilizopita. Inashauri wazazi hivi: “Waleeni [watoto] kwa fundisho la Kikristo katika nidhamu ya Kikristo.” (Waefeso 6:4, Phillips) Zaidi ya hilo, Neno la Mungu linatia moyo hivi: “Wakusanye watu, wanaume na wanawake na watoto . . . wapate kusikia na kujifunza.” (Kumbukumbu la Torati 31:12) Kanuni hizo zikitumiwa bila ugeugeu, hakika zitasaidia jamaa zijizuie zisivutwe na mwelekeo wa kubomoka wa jamii ya kisasa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki