Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 9/1 uku. 26
  • Unyofu Unawafanya Wawe Tofauti Pia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unyofu Unawafanya Wawe Tofauti Pia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • “Haiwezekani Mungu Kusema Uwongo”
    Mwimbieni Yehova Sifa
  • Kiapo cha Kale Ambacho Ni Muhimu Leo
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 9/1 uku. 26

Unyofu Unawafanya Wawe Tofauti Pia

ALIHUZUNIKA sana alipoona tiketi ya kumshtaki kwa sababu ya mahali alipoweka motokaa. Ilikuwa imewekwa penye kioo cha mbele. Faini ilikuwa dola 25 (za United States), naye aliumwa kwa sababu haikuwa haki. Hakukuwako ishara zo zote za kukataza kuweka motokaa hapo. Jambo la kusikitisha zaidi lilikuwa uhakika wa kwamba alikuwa ametoka mbali na hangeweza kurudi kwenye mji huo ili aombe rufani ya kesi hiyo Kwa hiyo akapiga picha za eneo hilo ili athibitishe hakuna sheria za kukataza zilizowekwa po pote. Na akiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova, akamuuliza Shahidi mwenzake aende mahakamani kwa niaba yake.

Hii ndiyo ripoti ya rafikiye kuhusu yale yaliyotukia mahakamani asubuhi hiyo:

“Unapoitwa mbele ya hakimu, unapaswa kusema jina lako na anwani. Kisha wanakulisha kiapo cha kusema ukweli. Kabla hawajanilisha kiapo, karani wa mahakama, mwanamume mzee, aliniuliza niseme tena anwani yangu ya barabara Niliposema, ‘124 Columbia Heights,’ ni wazi alitambua ilikuwa anwani ya makao makuu ya ulimwengu ya Sosaiti yetu na Mashahidi wa Yehova. Akimgeukia hakimu, akasema: ‘Usiwe na wasiwasi wo wote, Hakimu. Hawa ni watu wema! Hawasemi uwongo! Hawasemi uwongo kamwe! Hawawezi kusema uwongo! Dini yao hairuhusu kufanya hivyo, na wanaishikilia kabisa kabisa. Sijapata kujua ye yote wa wanaume wao wala hata wanawake wao akisema uwongo. Wao ni wanyofu kabisa. Nimeona mara nyingi wakati ambapo wangeweza kuepa kupata tiketi za kuwashtaki kwa ajili ya mahali walipoweka motokaa kwa kusema kiuwongo kidogo tu, lakini hawakufanya hivyo.’

“Halafu, akiniangalia, akasema, ‘najua huwezi kuniambia uwongo kwa sababu unajua ni nani angegutuka kaburini mwake kama ungefanya hivyo?’ ‘Ni nani huyo?’ nikauliza. ‘Yule Hakimu, Hakimu Rutherford [ambaye wakati mmoja alikuwa msimamizi wa Sosaiti yenu],’ akajibu. ‘Nilikuwa nikimpelekea barua miaka 47 iliyopita. Niliwajua Mashahidi wa Yehova kabla hawajaongezeka Hakimu huyo alikuwa mwanamume kweli kweli!’

“Baada ya hayo yote kusemwa, hakimu wa mahakama hata hakujisumbua kuniapisha. Aliniuliza nijitetee, nami nikafanya hivyo. Uamuzi? ‘Hakuna hatia.’”

Mashahidi wa Yehova ‘wanataka kujiendesha kwa unyofu katika mambo yote.’ (Waebrania 13:18, NW) Na kushikamana kwao na unyofu ni moja ya njia nyingi ambazo wanatofautiana na ulimwengu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki