Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 4/15 kur. 3-4
  • Hekima ya Mungu Je! Wewe Unaweza Kuiona?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hekima ya Mungu Je! Wewe Unaweza Kuiona?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hekima ya Yehova Yafanywa Idhihirike
  • Ile Hekima ya Kisilika ya Wanyama
  • Hekima ya Kimbingu ya Yehova
  • ‘Lo! Kina cha Hekima ya Mungu!’
    Mkaribie Yehova
  • Msifuni Mfalme wa Umilele!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • “Heri Mtu Yule Aonaye Hekima”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Je, “Hekima ya Kutoka Juu” Inakuongoza Maishani?
    Mkaribie Yehova
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 4/15 kur. 3-4

Hekima ya Mungu Je! Wewe Unaweza Kuiona?

ONA akilini mwako makao ya mfalme wa kale. Huko mfalme anaketi juu ya kiti chake cha ufalme cha utukufu asimamiapo, akiwa amepambwa mavazi ya kifalme. Yeye anajulikana sana si kwa sababu tu ya utajiri wake bali pia kwa sababu ya hekima yake. Watumishi wa makao yake wamepangwa kitengenezo kwa ukamilifu. Tamasha hiyo yenye uzuri mwingi inasisimua. Tazama: Mfalme Sulemani! —1 Wafalme 10:1-9, 18-20.

Msikilize, sasa, mwanamume anayetambuliwa kuwa aliye Mwalimu Mkuu Yesu Kristo: “Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti; nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.”—Mathayo 6:28, 29.

Yesu alimaanisha nini kwa maneno hayo. Basi, kwa hakika yeye alikuwa akitoa shauri juu ya kutokuwa mtafutaji wa mambo ya kimwili. Lakini je! maneno yake kuhusu Sulemani yangeweza kuwa ya kweli kihalisi? Kumbuka, Yesu alitumia mifano ya mambo ya kweli ya maisha. Kwa hivyo wabuni na mafundi wa Sulemani, ingawa walikuwa wenye ustadi, hawangeweza kutokeza ubuni unaolingana, mchanganyiko wa rangi, ulingano wa sehemu mbalimbali za “maua ya mashamba” yakiwa katika mazingira yao ya asili.

Hekima ya Yehova Yafanywa Idhihirike

Hata uchunguzi wa kijuujuu tu wa maua unaweza kufanya ukukubaliane na usemi wa Yesu. Sisi hatujui ni aina gani ya yungiyungi inayoelekea kuwa Yesu alikuwa nayo akilini, lakini maua yamejaa sana katika sehemu nyingi za dunia. Litazame ua kwa uangalifu, ua la aina yo yote: yungiyungi, waridi, au mmea wa aina nyingine wenye maua. Ni namna nyingi za rangi zenye kupendeza za ubuni wenye kutatanika kama nini unazoona, mchanganyiko wa vitawi vinavyoshikilia ua, majani yenyewe, na sehemu nyingine za mwili wa ua. Je! wewe unaweza kuona ushuhuda ulio kimya lakini wenye nguvu wa kwamba Mbuni Mkuu mwenye hekima isiyo na mwisho na wazo ndiye mwasisi wa kazi hiyo yenye kupendeza ya mikono? Macho yetu hayafurahii tu uzuri wayo bali pia matundu ya pua zetu huvuta manukato yayo yenye harufu nzuri-nzuri iliyo katika hewa tunayovuta.

Mtume Paulo alisema kwamba “sifa zisizoonekana [za Yehova] zinaonekana wazi tangu kuumbwa ulimwengu na kuendelea, kwa sababu zinafahamika kwa vitu vile vilivyofanywa.” (Warumi 1:20, NW) Hata hivyo, Mungu hakuumba tu maua ili kuipamba dunia; yeye aliumba vichaka na miti isiyohesabika, yote hayo yakifanyiza ufalme wa majani mabichi ulio na mafaa, lakini wenye kupendeza sana. Kama ungeweza kuzuru Msitu wa Kitaifa wa Humboldt katika Kalifornia, U.S.A., ungeweza kuona huko mti mwekundu ulio mkubwa mno unaoaminiwa kuwa ndio mti mrefu zaidi ulimwenguni. Kama ungeweza kusimama kwenye shina na kutazama juu kwenye urefu wa meta zaidi ya 110, je! wewe hungemsifu kwa ukimya Yeye ambaye alijua namna ya kuufanya mti kama huo?

Ile Hekima ya Kisilika ya Wanyama

Nchini na baharini mna wanyama, wadogo na wakubwa, ambao hutuvutia sana kwa hekima ya Mungu. Kwa wazi kila mmoja hutumikia kusudi fulani la Muumba. Sulemani mwenye hekima alishauri hivi: “Ewe mvivu, mwendee chungu, zitafakari njia zake ukapate hekima.” (Mithali 6:6) Wale ambao wamemtazama chungu wamestaajabia uwezo wake wa kupanga mambo. Chungu si wenye kujitenga na wengine; wao wanaishi jamii jamii. Wengine wao ni wakulima nao wanavuna mbegu. Katika nchi za tropiki unaweza kuwaona chungu fulani wakishughulika sana kuuma-uma vipande vya majani wapeleke kwenye matundu yao. Wanajuaje kufanya hivyo? Aguri, mmoja wa waandikaji wa kitabu cha Mithali, anajibu kwamba chungu wana “hekima kisilika.” Ni nani aliyewafanya hivyo? Ni Yehova, yule Mfanyizaji wa mbingu na dunia.—Mithali 30:24, 25, NW.

Ndiyo, viumbe-wanyama vina hekima kisilika. Inaonekana wazi sana katika kuhama kwa ndege. Huenda ukawa umesikia juu ya muhamo wa mbayuwayu wa Kapistrano. Wakati fulani kila mwaka, wao wanasafiri maelfu ya kilometa kutoka makao yao ya majira ya baridi katika Amerika ya Kusini kwenda San Juan Kapistrano katika Kalifornia, U.S.A. Kwa silika na bila kukosea wanakuja mahali pale pale wakati ule ule katika Machi.

Kwa habari ya ile bahari kuu, mtunga zaburi anasema: “Ee [Yehova], jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika.” (Zaburi 104:24, 25) Kuanzia na samaki wadogo wadogo mpaka nyangumi wakubwa, hekima ya kimungu inaonekana katika umbo na tendo lao.

Uumbaji wa Mungu wenye kukamilisha duniani ulikuwa mwanadamu mwenyewe. Hapa palikuwapo kiumbe ambaye hakutenda kwa kutumia tu hekima iliyotiwa ndani yake, au ya kisilika. Yeye alikuwa na uwezo wa kuwa kama Mungu katika njia nyingi. Ni kweli kama nini kuhusu yeye kwamba “kwa njia yenye kutia hofu” yeye ameumbwa kiajabu. Hata kama sisi si wanasayansi wa tiba, tunaweza kusoma mavumbuzi yao na kukata maneno kama yale ya mwandikaji aliyeongozwa kwa roho. Kazi za Muumba zinazodhihirishwa katika mwili wa kibinadamu ni za ajabu!—Zaburi 139:14, NW.

Hekima ya Kimbingu ya Yehova

Zaburi 19:1 inasema kwamba mbingu zinautangaza utukufu wa Mungu. Ni kweli sana kama nini! Mtunga zaburi Daudi hakuwa na darubini za kuona mbali au vifaa vingine vya kieletroniki, lakini yeye alikuwa na uthamini wa kuheshimu Mungu kwa yale aliyoweza kuona. Leo, mtu wa kawaida anajua mengi zaidi ya aliyojua Daudi juu ya mfumo wetu wa jua na galaksi yetu kubwa, ile Njia ya Kimaziwa. Pia anajua kwamba kuna galaksi kubwa nyinginezo zisizohesabika katika maeneo ya anga lisilo na mwisho. Wewe unahisije unapofikiria hekima ya Mbuni mkubwa na asiye na kifani? Je! wewe unaweza kusema kwa sauti yenye heshima ya kimungu: ‘Yehova, “[wewe unafanya] mambo makuu yasiyotafutikana; naam, mambo ya ajabu yasiyohesabika” ‘? Inakupasa kufanya hivyo. —Ayubu 9:10.

Katika enzi zisizojulikana zilizopita, Yehova aliendelea na matendo yake ya uumbaji, kwanza Mwanaye mzaliwa pekee, kisha ule uumbaji wake mwingine wa kiroho. Huo ulifuatwa na ulimwengu wa vitu vya kimwili. Kila kitu kilikuwa kitulivu na chenye utaratibu. Kwani, wana wa kimalaika wa Mungu kwa hakika walipaaza sauti zao za uthamini na kushangilia wakati wa kuwekwa kwa misingi ya dunia! (Ayubu 38:4-7) Mwanamume na mwanamke waliumbwa na kuwekwa katika shamba lenye ukamilifu, lakini ndipo jambo lenye kushtua likatukia. Sauti kutoka makao yasiyoonekana, ikisema kupitia nyoka, ikamchongea Muumba Mtukufu! Ilishtaki kwamba Yehova alikuwa akitumia vibaya enzi kuu yake; ikamwita Mungu mwongo. Hivyo, mwenyeji wa sauti hiyo alijipatia majina yenye kuchukiza yanayomtambulisha, kama vile Ibilisi, Nyoka, na Shetani. Sasa Yule Mwenye Hekima Yote angefanya nini? Angeweza kufanya nini? Kadiri mpya ya hekima ingehitajiwa ambayo ingepita mabuni ambayo tayari yamezidi fahari ya Sulemani. —Mwanzo 3:1-5.

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Kuanzia na samaki wadogo wadogo mpaka nyangumi wakubwa, hekima ya kimungu inaonekana katika umbo na tendo lao

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki